Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Jaji Mstaafu Januari Msoffe akimkabidhi Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Augostine Mahiga moja ya Ripoti tatu zilizofanyiwa utafiti na Tume hiyo kuhusiana na eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, Sheria ya Ushahidi na Sheria ya Ufilisi jijini Dodoma tarehe 13 Juni 2019. Kushoto ni Katbu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Profesa Sufini Msoffe. 
Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Jaji Mstaafu Januari Msoffe akitoa maelezo mbele ya Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Augostine Mahiga wakati wa kukabidhi Ripoti tatu zilizofanyiwa utafiti na Tume hiyo kuhusiana na eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, Sheria ya Ushahidi na Sheria ya Ufilisi jijini Dodoma tarehe 13 Juni 2019. Kushoto ni Katbu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Profesa Sufini Msoffe. 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Profesa Sufini Mchome akizungumza wakati wa makabidhiano ya Ripoti tatu zilizofanyiwa utafiti na Tume hiyo kuhusiana na eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, Sheria ya Ushahidi na Sheria ya Ufilisi jijini Dodoma tarehe 13 Juni 2019. 


Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Jaji Mstaafu Januari Msoffe akimkabidhi Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Augostine Mahiga moja ya Ripoti tatu zilizofanyiwa utafiti na Tume hiyo kuhusiana na eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, Sheria ya Ushahidi na Sheria ya Ufilisi jijini Dodoma tarehe 13 Juni 2019. (PICHA NA MUNIR SHEMWETA) 

…………………………………………………………… 

Na Munir Shemweta, Dodoma 

Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania imekabidhi Ripoti ya Mapitio ya Sheria ya eneo la hifadhi ya Ngorongoro lilipo mkoani Arusha kwa Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Agostine Mahiga. 

Aidha, Tume imekabidhi pia Ripoti mbili za Sheria ya Ufilisi na ile ya Ushahidi ambazo zote kwa pamoja zimekabidhiwa kwa Dkt Mahiga na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Jaji Mstaafu Januari Msoffe leo tarehe 13 Juni 2019 jijini Dodoma. 

Akizungumza wakati wa kukabidhi Ripoti hizo, Mwenyekiti wa Tume Jaji Mstaafu Januari Msoffe alisema Tume yake imeamua kufanya utafiti wa eneo la hifadhi ya Ngorongoro baada ya kuombwa na Mamlaka ya Ngorongoro kufanya utafiti kutokana na eneo hilo kuruhusu matumizi mseto ambapo Wanyama pori, Mifugo na Binadamu wanaishi eneo moja. 

Jaji Mstaafu Msofe alisema, eneo la Hifadhi ya Ngogongoro ni hifadhi ya pekee inayoruhusu matumizi mseto yanayojumuisha watu, mifugo na wanyama pori na kusisitiza kuwa Tume yake wakati wa kupitia sheria hiyo imebaini upungufu wa kisheria na kiutendaji. 

Alisema, katika utafiti huo Tume ya Kurekebisha Sheria ilibaini ongezeko kubwa la idadi ya watu katika mhifadhi hiyo ambapo mwaka 1959 hifadhi hiyo ya Ngorongoro likuwa na idadi ya watu 8,000 wakati sasa ina takriban wakazi 93,000 jambo alilolieleza kuwa linahatarisha kupungua kwa malisho ya wanyama, uharibifu wa mazingira pamoja na kuharibiwa kwa mapito ya wanyama. 

Aidha, Mwenyekiti huyo wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania alisema, hifadhi hiyo ya Ngorongoro pia imeathiriwa na usajili wa vijiji ndani ya hifadhi pamoja na ujangili jambo alilosema limesababisha kupungua wanyama pori wakiwemo Faru na Mbwa mwitu. 

Jaji Mstaafu Msoffe aliongeza kwa kusema, Tume yake inapendekeza hatua za kuangalia mfumo wa matumizi Mseto katika hifadhi ya Ngorongoro kwa lengo la kuhakikisha eneo hilo linakuwa endelevu. 

Kwa upande wake Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Agostine Mahiga aliipongeza Tume ya Kurekebisha Sheria kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kufanya tafiti katika sheria mbalimbali na kueleza kuwa chombo hicho ni muhimu katika nchi kwa kuwa kinabeba majukumu ya masuala ya sheria ili yasije kupitwa na wakati na kubainisha kuwa Tume ina macho matatu katika utendaji wake ambapo inaangalia sheria zilizopo, zilizopita na zijazo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...