NA MWAMVUA MWINYI, PWANI
JESHI la polisi mkoani Pwani, linawashikilia wahamiaji haramu sita ambao ni raia kutoka nchini Ethiopia kwa kosa la kuingia nchini bila kibali, huku likikamata watu wengine 29 kwa kujihusisha na matukio ya uvunjaji nyumba usiku na kuiba.

Watuhumiwa hao wamekamatwa kufuatia msako mkali na oparesheni dhidi ya vikundi vya vijana wa mitaani wanaojihusisha na wizi kwa kuvunja, kupora na kukaba raia wema huko wilaya ya kipolisi Chalinze .

Akielezea kuhusiana na matukio hayo,kamanda wa polisi mkoani Pwani Wankyo Nyigesa alisema baadhi yao walikamatwa wakiwa na mali kadhaa,madawa ya kulevya aina ya bangi kete 142,puli nne,pombe haramu ya moshi lita 25 na pikipiki moja.

Anabainisha kwamba, pia kumekamatwa magunia 90 ya mkaa uliovunwa bila uhalali ,mashuka,raba,vitenge,mafuta ya pikipiki na mafuta ya kula yanayodaiwa kuingizwa kwa kukwepa ushuru lita 300.

Akizungumzia kuhusu wahamiaji haramu alisema ,watafikishwa katika idara ya uhamiaji kwa taratibu nyingine za kisheria. Kamanda huyo alitoa rai kwa jamii ,kuwa itambue uhalifu haulipi na hauna faida kwani siku za mwizi ni arobaini na akishikwa mtu akijihusisha na uhalifu atakiona.

Vilevile anawataka walioibiwa kufika katika kituo cha polisi Chalinze kutambua mali zao .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...