Na Woinde Shizza Michuzi Tv , Arusha 

WANANCHI wenye tabia ya kulalamika kuwa hawana kazi pamoja na kudai kuwa maisha magumu wameshauriwa kuchangamkia fursa mbalimbali zinazopatikana ili kujipatia kipato na kukuza uchumi wa nchi.

Ushauri huo umetolewa na Mtume Sekela Lolandi wa Huduma ya Ngurumo ya Upako wakati akizungumzia na waumini wa huduma ya Ngurumo ya Upako Ndani ya hema la kukutania la Chuo cha Unabii Kisongo mkoani Arusha .

Amesema kuna Watanzania wengi wamekua na tabia ya kukaa tu bila kufanya Kazi na kuitupia lawama Serikali kitu ambacho sio kizuri kwani kila mtu aliumbwa akiwa na ujuzi wake ambao akijiongeza hatakosa fedha wala kazi ya kufanya. 

"Baadhi ya watanzania haswa wanaosema mmesoma mmekuwa na tabia mbaya sana ya kulala mikia Serikali kuwa haiwapi kazi kitu kinachonifanya nishangae.

"Wengine wanaona kabisa nikifanya hivi naweza nikapata fedha na maisha yakaenda lakini kwavile anajiona amesoma anaacha kufanya na kujihisi watu watamshangaa kitu ambacho ni cha ajabu,"amesema.

Amefafanua kuwa kazi yoyote ni nzuri mradi iwe halali na inakubalika na sheria za nchi yetu huku akisisitiza wananchi hasa vijana wasikae wakisubiria kuajiriwa bali wajiajiri wenyewe kwa kufanya kazi 

"Mnajua hata vitabu vya dini vimeandika asie fanya kazi asile sasa wewe umekaa kwa jirani kuna kibarua cha kufua badala ukafue upate fedha unasema mimi na elimu yangu nikafue .Kazi ni kazi, hivyo tufanye kazi kwani unaweza kufua nguo za jirani na baadae utafungua kiwanda,"amesema.

Kwa upande wake Nabii Mkuu Dk.Geordavie Kasambale wa Huduma ya Ngurumo ya Upako Arusha amesema kwa sasa hivi sio muda wa wananchi na hasa vijana kukaa na kujibweteka huku wakilalamika hakuna kazi bali ni muda wa kuamka na kuanza kuchangamkia fursa zilizopo. 

"Kuna mambo yanahitajika na yanafursa kubwa, kwa mfano kipindi hichi kuna uhitaji wa mifuko ambayo sio ya Plastiki, nenda tafuta anaejua kutengeneza tengeneza leta sokoni uza na si kukaa na kulalamika Serikali haikusaidii,"amesema.

Ameongeza nchi ya Tanzania ni nchi yenye fursa nyingi za kujipatia kipato lakini baadhi ya wananchi wamebaki kuwa maskini kutokana na kutofanya kazi na kubaki kuitupia lawama Serikali , jambo ambalo si sahihi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...