Airtel yatoa msaada wa kitanda cha oparesheni Hospitali ya Mkuranga
Ni muendelezo wa kampeini ya Airtel Tunakujali ambapo wafanyakazi wa kampuni huchangia kipato chao kusaidia vikundi mbali mbali katika Jamii wenye uhitaji maalum

MKURANGA, KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kupitia kitengo chake cha Huduma kwa wateja wakubwa wameshiriki kampeni maalum yakusaidi jamii inayojulikana kama Aitel Tunakujali kwa kutoa msaada wa kitanda cha kufanyia upasuaji (oparesheni) kwa kwa akinamama wanojifungua kwenye thamnai ya Sh. Milioni tano kwa hospitali ya wilaya ya Mkuranga mkonini Pwani.

Airtel Tunakujali ni programu maalum ambapo wafanyakazi wa kampuni hiyo huchangia sehemu ya kipato chao kwa ajili ya huduma za kijamii zikiwemo afya na elimu.

Akizungumza jijini wilayani Mkurranga wakati wa hafla fupi ya kukabidhi msaada huo wa kitanda mwishoni mwa wiki, Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema kuwa kitengo cha kuhudumia wateja wakubwa Airtel kiliandaa hafla kwa ajili ya kuchangia fedha kwa ajili ya kulipia bima ya afya ya watoto ambao wazazi wao hawana uwezo wa kulipia matibabu na tayari watoto hao washalipiwa bima kwa mwaka mzima.

‘Hapa leo tufanya muendelezo wa kuendelea kusaidia huduma ya afya. Kwa leo tunakabidhi hiki kitanda cha upasuaji kwa akinamama wanaojifungua. Hii inatokana na kuelewa ya kwamba hospitali hii ina changamoto nyingi na upungufu wa vifaa vya hospitali huku hiki kitanda kikiwa ni moja wapo. Sisi Airtel tuna uhakika ya kwamba kitasaidia wale akina mama waliokuwa na utahitaji wa upusuaji lakini wanakosa huduma kama hii. Tunaomba uongozi wa hospitali ukitunze vizuri na sisi Airtel tunahidi kuendelea kusaidia kwenye huduma za afya na zingine zenye kugusa jamii yetu moja kwa moja, Mmbando alisema.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Dkt Stephen Mwandambo mbali na kutoa pongezi kwa Airtel alisema kuwa hospitali ya wilaya ya Mkuranga inakabiliwa na changamoto kadhaa huku akitoa mfano kuwa hospitali hiyo ina uwezo wa kuhudumia wakinamama waokuja kujifungua kwa wastani wa 70 kwa mwezi lakini kwa hali halisi imekuwa ikihudumia 270 mpaka 400.

‘Kulingana na idadi hiyo kubwa ya wakinamama ambao wanapata huduma ya kufingulia kwenye hospitali yetu ya wilaya tumekuwa tukipata changamoto nyingi huku tukiwa na kitanda kimoja tu kwa ajili ya upasuaji. Kwa msaada huu kutoka Airtel itasaidia sana sisi pamoja na kupunguza wa vifo vinavyotokana na kukosa kitanda hiki, alisema Dkt Mwandambo huku akiongeza kuwa hospitali hiyo imekuwa ikitoa huduma ya matibabu kwa wakazi wa wilaya ya Mkurunga asilimia 80 na asilimia 20 wanatoka wilaya za Kibiti na Temeke.

Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya ya Mkurunga Injinia Mshanu Munde akipokea msaada huo kwa niaba ya serikali ya wilaya alitoa pongezi kwa Airtel na hasa wanafanyakazi ambao waliweza kutoa sehemu ya kipato chao na kufanikisha upatikanaji wa kitanda hicho.

Sisi zote tunajua kampuni ya Airtel ni ya kizalendo kwa inamilikiwa na wananchi kupitia serikali yao kwa asilimia 49. Lakini naomba niwapongezi wanafanya kazi kitengo cha kuhudumia wateja wakubwa na uzalendo wao wa kuona umuhimu wa kuimarisha sekta ya afya na kuamua kwa hiari yao kutoa sehemu ya mapato yao na kuweza kufanikisha jambo hilo. Na wakaribisha kwenye wilaya yetu lakini tuna changamoto nyingi kwenye sekta hizi mbili za afya na elimu nawaomba mkipata nafasi siku nyingi kuja na kuendelea kutuunga mkono alisem Injinia Munde.

Meneja wa Kitengo cha kuhudumia wateja wakubwa Airtel Tanzania Alice Maziku akimkabidhi kitanda cha upasuaji Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Mkuranga Injinia Mshanu Munde mwishoni mwa wiki. Kampuni ya Airtel Tanzania kupitia mradi wa AIRTEL TUNAKUJALI ilitoa kitanda cha upasuaji kwa wakinamama wanaojifungua kwa hospitali ya Mkurunga ikiwa ni juhudi za kusaidia jamii iiliyo kwenye mahitaji maalum. Wengine ni Mganga Mkuu wa wilaya ya Mkuranga Dkt Stephen Mwandambo (kati kati), Meneja Uhusiano Airtel Tanzana Jackson Mmbando (wa kwanza kulia) na katibu wa Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Omari Kisali (wa kwanza kulia).
Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando (kulia) akisalimiana na Injinia Mshanu Munde baada ya Airtel kukabidhi kitanda cha upasuaji kwa hospitali ya wilaya ya Mkuranga mwisho mwa wiki. Airtel ilitoa kitanda hicho kwenye thamani ya Milioni tano ikiwa ni juhudi za kusaidia jamii kupitia mradi wa AIRTEL TUNAKUJALI. Wengine ni Wengine ni Mganga Mkuu wa wilaya ya Mkuranga Dkt Stephen Mwandambo (kati kati) na katibu wa Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Omari Kisali (wa kwanza kulia).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...