Charles James

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dk Augustine Mahiga amefunga zoezi lilioanza Julai mwaka huu la kupitia mfumo wa haki jinai ili kuufanyia maboresho.

Dk Mahiga amesema Wataalamu kutoka Wizara, Taasisi za Serikali na Asasi za kiraia wamekua wakichambua na kujadili masuala mbalimbali katika mfumo wa haki jinai ambayo yamekua kikwazo katika kushughulikia na kusimamia masuala ya kijinai nchini.

" Kazi hii imefikia hatua ambayo mtapitishwa na kujadili maeneo yaliyopendekezwa kuboreshwa ili kuifanya mfumo huu kuwa rafiki Kwa wadau wa haki jinai," amesema Dk Mahiga.

Amesema mfumo huo kwa ujumla unahusisha mnyororo wa hatua mbalimbali zinazotokea wakati wa kushughulikia uhalifu kuanzia katika ngazi ya kuzuia uhalifu usitokee, kutambua unapotokea m, kukamata wale wanaofanya uhalifu, kupeleleza, kushitaki mahakamani na kutoa adhabu.

Katika mnyororo huo mambo mbalimbali yamewekwa kisheria ya namna ya kushughulikia wahalifu ambayo yanashughulikiwa na vyombo au Taasisi mbalimbali za jukwaa la haki na jinai.

Mara ya mwisho kupitia mfumo huo n kuufanyia maboresho ni takribani miaka 20 iliyopita hivyo ni muhimu kupitia mfumo huo na kuufanyia maboresho ili kuendana na wakati uliopo." Niwapongeze wataalamu wetu ambao mmekua hapa kwa miezi miwili na wote ambao mmeshiriki katika kazi hii hadi hatua hii ya leo.

" Niwashukuru Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala Mikoa kwa kutenga muda wao kutembelea wakati wa mchakato wa maboresho haya kwa ngazi ya watalaamu. Nimshukuru pia Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally ambaye nae alitenga muda wake na kutembelea wataalamu wakati wa mchakato," amesema Dk Mahiga.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Augustine Mahiga akizungumza wakati wa hitimisho la mchakato wa maboresho ya sekta ndogo ya haki jinai.
 Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Augustine Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa mchakato wa maboresho wa sekta ndogo ya mfumo wa haki jinai. Kushoto kwake ni Waziri wa Nchi Utumiahi, Kepteni George Mkuchika na kulia ni Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...