PICHA NAMBA 1
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, kuhusu maamuzi ya Serikali katika utekelezaji wa madeni yanayodaiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), kwa wadaiwa sugu mjini Dodoma.
PICHA NAMBA 2
Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya Sekta hiyo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, mjini Dodoma.
PICHA NAMBA 3
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mheshimiwa Selemani Kakoso, akizungumza na Viongozi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na Watendaji wa Taasisi zilizo chini ya Sekta ya Ujenzi mara baada ya kupokea taarifa ya Utekelezaji wa Sekta hiyo, mjini Dodoma.
PICHA NAMBA 4
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Viongozi na Watendaji wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na Taasisi zilizo chini yake, wakiwa katika kikao kilichohusisha uwasilishaji taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya kamati hiyo, mjini Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...