Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Uongozi wa Klabu ya Yanga umeteua wajumbe tisa watakaouunda kamti ya Sheria na nidhamu.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Dkt Mshindo Msolla wa kuunda tume hiyo itakayoongozwa na Mwenyekiti wake Adv Sam  Mapande.

Aidha, wajumbe  ni Cosmas Chidumule, Esther Cheyo, Sharifu Makosa, Benjamin Mgonja na Philipo Bura.

Wengine ni Seleman Jongo na Mary Mavula  ambapo wote kwa pamoja wataunda kamati hiyo itasimamia sheria na nidhamu ndani ya klabu hiyo.

Kwa sasa Yanga inaendelea kuboresha baadhi ya kamati zao ili kuboresha utawala bora ndani ya klabu hiyo.

Timu ya Yanga ina mchezo wa mkondo wa pili wa Klabu Bingwa dhidi ya Township Rollers nchini Botswana siku ya Jumamosi ambapo Yanga inahitajika kushinda mchezo huo au kupata sare ya kuanzia goli 2 na kuendelea ili kufanikiwa kutinga hatua inayofuata.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...