Mkurugenzi wa Biashara ya DCB , James Ngaluko (katikati)akizungumza mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati benki hiyo benki hiyo ikitangaza kutangaza kumaliza kampeni ya bidhaa yake ya akaunti ya muda maalumu inayojulikana kama ‘DCB Lamba Kwanza’ kwa mafanikio makubwa. Kampeni ya DCB Lamba Kwanza ilizinduliwa Mei 29 mwaka huu na kudumu kwa muda wa miezi mitatu.


Na Said Mwishehe, Michuzi TV
MKAKATI wa Serikali ya Awamu ya Tano kuimarisha taasisi za fedha ikiwemo sekta ya kibenki umeendelea kuungwa na Benki ya Biashara ya DCB kwa kuhakikisha inaendelea kutoa huduma bora za mikopo na zenye riba nafuu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa benki hiyo James Ngaluko amesema pamoja na mambo mengine wanatambua jitihada za Serikali za kuhakikisha Watanzania wanapata huduma bora na zenye gharama nafuu ikiwemo mikopo na wao wamekuwa mstari wa mbele kuunga mkono jitihada hizo kwa kuwahudumia Watanzania.

"Tunatambua ambavyo Serikali inazungumzia umuhimu wa kuboreshwa kwa huduma za kibenki ikiwemo ya kutoa mikopo kwa haraka na yenye riba nafuu.

"Serikali imekuwa ikihimiza riba kupungua nasi tumepunguza riba zetu kwa kiwango kikubwa, nia yetu ni kuona kila Mtanzania anajenga uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla,"amesema.

Wakati huo huo Ngaluko amesema kampeni ya bidhaa yao ya akaunti ya muda maalumu inayojulikana kama ‘DCB Lamba Kwanza’ imekuwa na mafanikio makubwa kwani imevuka malengo yake iliyojiwekea ya Sh.bilioni 15 na kuongeza amana kwa Sh.bilioni 18.5 ambayo ni zaidi ya asilimia 123.

"DCB Lamba Kwanza ilizinduliwa Mei 29 mwaka huu na kudumu kwa muda wa miezi mitatu huku ikiwa na lengo la kukusanya amana za kiasi cha Sh.bilioni 15, iliwawezesha wateja wetu kupata riba ya hadi asilimia 14 ya amana wanayowekeza  ambapo mteja alianza kupokea riba yake ya mwezi  papo hapo,"amesema.

Ngaluko amesema wanatoa shukrani kwa wateja wao kwa kuipokea bidhaa hiyo na kuweza kunufaika nayo kwani kila mwezi umekua ni wa faida.Mteja anafurahia riba yake inayolipwa mwanzo wa mwezi kila mwezi.
Amesema malipo ya riba ni rafiki kuwa kuwa mteja anaweza kuwekeza kuanzia miezi mitatu mpaka miaka miwili na ni jambo la fahari kuona benki ya kitanzania inatoa fursa kwa Watanzania na kuwawezesha kuboresha maisha na uchumi.

Hata hivyo amesema DCB Lamba Kwanza imepokewa kwa mikono miwili na wateja wetu na kufanikiwa kuvuka malengo kwa kukusanya amana ya zaidi ya Sh.bilioni 18.5 ambapo awali Benki ilikusudia kuuza kiasi cha Sh. bilioni 15.

"Tunawashukuru wateja wetu kwa kuendelea kutuunga mkono kwa kila bidhaa tunayoiingiza sokoni na kutuwezesha kuvuka malengo hii inaonyesha ni jinsi gani DCB inavyo aminika kwenye soko.Tupo imara na tumejidhatiti katika kubuni na kuingiza bidhaa zitakazokidhi kiu ya mahitaji ya huduma za kifedha kwa wateja wetu,"amesema.

Pia amesema benki hiyo imeendelea kufanya maboresho katika baadhi ya huduma zake ikiwa ni pamoja na kupunguza riba na kuongeza muda wa marejesho hadi miaka 15 kwa mikopo ya ujenzi na ununuaji wa nyumba za makazi kwa wateja wetu wote hususan wafanyabiashara na waajiriwa. 

Ametumia nafasi hiyo kutoa mwito kwa wajasiriamali wote na wafanyakazi wenye lengo la kununua au kujenga nyumba kuwahi fursa hii. Pia amesema benki inatoa huduma za kidigitali kupitia DCB DIGITAL inayomuwezesha mteja kufungua akaunti kupitia simu yake ya mkononi.

Pamoja na hayo,Ngaluko amesema kuwa  benki hiyo imeendelea kupata faida, na kufikia kipindi cha nusu ya kwanza ya  mwaka huu imeweza kupata faida ya Sh.bilioni 1.2 ikiwakilisha ongezeko la asilimia 118  kutoka faida ya kipindi kama hicho kwa mwaka 2018.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...