Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Dkt. Kiagho Kilonzo akizungumza na waandishi habari katika maonesho ya Tamasha la Utamduni wa Juimuiya ya Afrika Mashariki (Jamafest)linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Nchini Dkt.Kiagho Kilonzo ameutaka umma wa watanzania kutembelea bodi ya Filamu katika tamasha la Utamaduni wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (Jamafest) katika kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na bodi hiyo.
Kaimu Katibu Mtendaji Dkt.Kilonzo ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi habari katika maonesho hayo na kuwaasa watanzania kutumia chombo hicho katika kukuza sanaa ya filamu nchini kwa kuleta maendeleo.
Amesema kuwa katika maonesho hayo wataona vitu mbalimbali ambavyo vimefanywa na watanzania kwa kutengeneza filamu ambazo zina maadili na pale ambapo wanaona filamu zilizozalishwa hazina maadili wanachukua hatua kuhakikisha hazionyeshwi.
Dkt. Kilonzo amesema kuwa maonesho hayo ni fursa kwa Tanzania na kuona namna ya nchi wanachama wengine wanavyofanya utamduni wao huku wakijifunza utamduni wetu.
"Natarajia wataopita katika banda la bodi ya filamu watajifunza vitu vingi ambavyo vitawasaidia kuingia katika sekta ya filamu na kuweza kuzalisha ajira zao pamoja na taifa kupata maendeleo katika sekta hiyo"amesema Dkt. Kilonzo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...