Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Phaustine Kasike, akisalimiana na Naibu Kamishna wa Magereza, Afwilile Mwakijungu mara baada ya kuwasili kwenye Viwanja vya Nanenane, Mkoani Mororogoro tayari kwa Kikao Maalum cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo. Kikao hicho kimefanyika kwa siku moja leo 28 Septemba, 2019 Mkoani Morogoro.
Kamishna wa Huduma za Urekebishaji na Urekebu, Tusekile Mwaisabila akitoa utambulisho mfupi wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza kabla ya kumkaribisha Kamishna Jenerali wa Magereza kufungua rasmi kikao kazi hicho.
Wajumbe wa Kikao hicho ambao ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa makini maelekezo kutoka kwa Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike (hayupo pichani).
Mkuu wa Magereza Mkoani Lindi, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Josephine Semwenda(kushoto), Mkuu wa Magereza Mkoani Geita, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Edith Mbogo(katikati) na Mkuu wa Magereza Mkoani Pwani, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rehema Ezekiel kwa pamoja wakiteta jambo mara baada ya ufunguzi wa Kikao kazi cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza ambacho kimefanyika kwa siku moja leo 28 Septemba, 2019 Mkoani Morogoro.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Phaustine Kasike akitoa hotuba ya ufunguzi wa Kikao Maalum cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza leo 28 Septemba, 2019 Mkoani Morogoro.
Meneja wa SACCOS ya Magereza(TPS SACCOS), Kamishna Msaidizi wa Magereza, Abdallah Missanga akitoa ufafanuzi wa huduma mbalimbali zinazotolewa na Chama hicho cha Ushirika cha Jeshi la Magereza mbele ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...