Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Philip Mpango amesema kuwa Chuo cha Usimamizi wa Fedha kwnda kwa kasi katika teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwani mafisadi na Wezi wanakwenda kidigitali kujipatia fedha hivyo lazima rasilimali watu wa kutosha katika teknolojia.

Waziri Mpango aliyasema hayo wakati akizundua Baraza la Uongozi wa Chuo hicho lilofanyika jijini Dar es Salaam, amesema  kuwa masoko ya mitaji, dhamana na bidhaa nayo lazima yaanze kuangaliwa kwa mtazamo mpya kwa kuwa aina za huduma za kifedha kunyumbulika kwani  wahalifu, wakiwemo mafisadi, wezi wa fedha za umma na matapeli, wameanza kwenda kidigitali.

Dkt.Mpango amesema IFM ni muhimu ianze kujielekeza kuchangamkia fursa na pia kujibu changamoto zinazoambatana na uchumi wa kidigitali ambako ndiko dunia inakoelekea kwa kasi licha ya kukua kwa miamala kupitia simu za kiganjani na kompyuta tayari pia zipo sarafu za kidigitali na miamala mikubwa inafanyika kwa njia hizi hivyo hakuna chaguo bali ni lazima kuanzia sasa mafunzo na utafiti unaofanyika hapa IFM ujielekeze kufungulia ubunifu na uvumbuzi wa vijana wa kitanzania utakaowawezesha kuelewa mabadiliko hayo.

Amesema kuongoza vema sekta ya fedha katika mazingira ya muunganiko wa kidigitali katika sekta ya fedha kitaifa na kimataifa na pia ushindani mkali  kwani hakuna budi kuangalia upya uhasibu na namna ya kuandaa vitabu vya mahesabu na ukaguzi wa miamala ya fedha katika mazingira haya mapya. Kadhalika, masomo ya tasnia ya kibenki na bima.

Dkt.Mpango amesema kila mmoja aliyeuliwa katika baraza hilo ni kwa sababu Serikali imejiridhisha kwamba mnao ujuzi, weledi, uzalendo na uzoefu mkubwa katika uongozi.

 Aidha amesema  kuwa wajube wa baraza wanajua na kuthamini mchango mkubwa wa taasisi za elimu ya juu katika nchi kupitia kazi zake za msingi za kufundisha, kufanya utafiti na kutoa ushauri hivyo, Serikali ina matarajio makubwa kwamba Baraza kweza kukisimamia chuo vizuri.

“Baraza lipeleke cha IFM na mbele zaidi ili kiweze kutoa mchango mkubwa kuliko ilivyo sasa katika maendeleo ya Taifa letu. Tutashangaa sana kama atatokea mmoja wenu akaja kubainika baadaye kwamba anatumia uwepo wake kwenye Baraza kusimamia maslahi binafsi au ya kundi fulani badala ya maslahi mapana ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha na Taifa kwa ujumla”amesema Dkt. Mpango.

“Katika kutekeleza yote panahitajika ushirikiano mzuri na wa karibu sana kati ya Baraza la Uongozi na Menejimenti ya Chuo  hivyo, napenda nisisitize kuwa mivutano isiyo na tija kati ya Baraza na Menejimenti ya Chuo ama ndani ya timu ya menejimenti ya Chuo chetu adhimu isipatiwe nafasi kabisa”amesema Dkt Mpango.

Amesema Baraza lione umuhimu wa kukiongoza Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kwa kuweka jicho la pekee katika maeneo mawili. Kwanza, ni kujitathmini kama kweli elimu inayotolewa katika Chuo hiki na wahitimu wa Chuo hiki vinakidhi mahitaji ya kujenga uchumi wa viwanda na kuibadilisha Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati itakapofika mwaka 2025 na kuendelea kujenga nchi ya kipato cha juu.

Dkt. Mpango amesema Serikali ya awamu ya tano ni kwamba Chuo hiki kitaendelea kusimamia vizuri maandalizi ya rasilimali hii adhimu ya Usimamizi wa Fedha, itakayokidhi mahitaji ya uchumi wa kati unaongozwa na Sekta ya viwanda ifikapo mwaka 2025.

Nae Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha Profesa Tadeo Satta amesema Chuo kinafanya tafiti na huduma za ushauri services) kwa jamii katika fani za usimamizi wa fedha, uhasibu, benki, bima, kodi, hifadhi za jamii, teknolojia ya mawasiliano ya habari (ICT), sayansi ya komputa na nyinginezo.

Amesema chuo cha Usimamizi wa Fedha kimedhamiria kuwa Kituo Bora cha Mafunzo kwa Taaluma na Utaalamu na vile vile kuleta chachu ya mabadiliko katika fani za fedha na zinazoshabihiana

Katika Mpango Mkakati wa Chuo kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 – 2020/2021 Chuo kimeainisha malengo yafuatayo ambayo yanaendelea kutekelezwa kuboresha mafunzo ya kitaaluma na kitaalamu, utafiti na ushauri elekezi, Kuimarisha Uwezo wa Utendaji wa Rasilimali Watu na zana za kufanyia kazi, Kuboresha mifumo ya utawala bora na uongozi,Kuimarisha Uwezo endelevu wa Fedha,Kuboresha Huduma za Afya na kupunguza maambukizi ya VVU na UKIMWI pamoja ,Kuzingatia na kuendeleza Mkakati wa Taifa wa kupambana na rushwa na mpango wa utekelezaji wa Mkakati huo.

Mwenyekiti wa Baraza hilo Balozi Dkt.Benson Bana amesema changamoto katika chuo hicho watazifanya kuwa fursa katika kufanikisha matarajio ya serikali katika ujenzi wa uchumi wa viwanda.
 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Philip Mpango katikati akizungumza wakati akizundua Baraza la Uongozi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha Profesa Tadeo Satta akitoa maelezo kuhusiana na mikakati ya chuo hicho katika uzinduzi wa baraza la uongozi wa chuo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa baraza la Uongozi wa Chuo hicho Balozi Dkt.Benson Bana akitoa maelezo kuhusiana na baraza lilivyojipanga katika kutekeleza majukumu ya kusukuma chuo katika uzinduzi wa baraza hilo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Uongozi na Menejimenti ya IFM wakiwa kwenye mkutano huo
 Picha ya Pamoja na Baraza la uongozi na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango
Picha ya Pamoja Menenejimenti ya IFM na Waziri wa Fedha na Mipango 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...