Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeifungia Kwanza TV kwa kipindi cha miezi sita ili waweze kujirekebisha katika uendeshaji luninga katika mitandao.
Kwanza TV walikutwa na kosa la kuchapisha habari iliyokuwa inamuhusu Dkt.Gwajima kupata ajali ya gari ambapo katika utetezi wao walidai kuwa taratibu za kihabari zilifuatwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui Joseph Mapunda amesema kuwa Kwanza Tv walikutwa na makosa ya habari ya ajali ya Dkt.Gwajima ambayo haikufafanunua ni Gwajima yupi ambapo ni kosa katika uandishi.
Amesema Kamati hiyo ilisema kuwa ajali hiyo ilikuwa inamhusu Katibu Mkuu wa Tamisemi Afya Dkt.Doroth Gwajima hivyo kulifanya watu wengine kushindwa kujua ni Dkt.Gwajima gani kutokana na kutokwepo kwa majina yote.
Aidha Kamati hiyo imetoa faini ya sh.milioni tano kwa Ayo na Watetezi TV kwa kila mmoja kulipa fedha hiyo kwenye mamlaka hiyo kutokana na kushindwa kuchapicha Sera ya maudhui na miongozo katika luninga zao na kuweza kuona watazamaji. Mapunda amesema vyombo vya habari vifuate taratibu , kanuni na sheria katika kutangaza au kuhabarisha umma kwa kuzingatia misingi ya uandishi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...