Mkemia Mkuu wa Serikali Dk.Fidelice Mafumiko akizungumza na waandishi wa habari katika semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kwaajili ya kuandika habari sinazohusu Mamlaka ya Maabara ya Mkemia mkuu wa Serikali jijini Dar es Salaam.

Na Said Mwishehe,Michuzi Blogu
MAMLAKA ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali(GCLA) imesema imeanza mchakato wa awali wa kuhakikisha kunakuwa na Kanzi Data kwa ajili ya kutunza vinabasa vya kila Mtanzania.

Kauli hiyo ya mamlaka hiyo imekuja baada ya Michuzi Blog na Michuzi TV kutaka kufahamu kuna mkakati gani wa kuanzishwa Kanzi Data kwa ajili ya kutunza vinasaba vya Watanzania wote kutokana na umuhimu wake.

Kwa mujibu wa mamlaka hiyo, vinasaba ndio vimebeba taarifa zote muhimu za binadamu yoyote na kila mmoja anavinasaba ambavyo havifanani na mtu mwingine.

Kwa kukumbusha tu jana Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ilikuwa imeandaa mafunzo kwa waandishi wa vyombo vya habari nchini kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kuifahamu mamlaka hiyo na majukumu yake ili wanapoandika habari zinazohusu mamlaka kuwa na uelewa wa kutosha.Mafunzo kama hayo yametolewa pia kwa wahariri wa vyombo vya habari mwoshoni mwa wiki iliyopita.

Wakati anajibu swali hilo, Mkemia Mkuu wa Serikali Dk.Fidelice Mafumiko amesema tayari Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu imeanza mchakato wa awali kwa ajili ya kuanzisha kanzi data ya kutunza vinasaba.

"Tunafahamu umuhimu wa vinasaba , hivyo kutokana na umuhimu wake tupo katika hatua za mwanzo kabisa za kuanzisha kanzi data ili kuhifadhi vinasaba vya kila mtu.Tunapozungumzia hatua za awali ni pamoja na kuwa na hilo wazo ambalo tayari tumeanza kulifanyia kazi,"amesema Dk.Mafumiko.

Amefafanua pamoja na kuwa katika mchakato wa kuanzisha kanzi data hiyo, ukweli uliopo sampuli zote za vinasaba ambavyo vimekuwa vikienda ofisi ya mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu wa Serikali vimekuwa vikihifadhiwa na vyote vipo."Vinasaba vyote ambavyo vimekuja kwetu na kupima tunavyo hivyo kuna mahali pakuanzia.".

Dk.Mafumiko amesema ni muhimu kuwa na kanzi data kwani itasaidia kurahisisha mambo mbalimbali yanayohitaji uchunguzi wa vinasaba na kutoa mfano kuwa ajali iliyotokea mkoani Morogoro kwa watu kadhaa kuteketea kwa moto iwapo kungekuwa na kanzi data ya vinasaba basi ingekuwa rahisi sana ndugu kutambua miili ya ndugu zao.

Awali Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Kemikali katika mamlaka hiyo Danile Ndiyo amesema kuwa ni marufuku kwa mtu yoyote ambaye hajasajaliwa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kutoa mafunzo yanayohusu masuala ya kemikali.

"Ni marufuku kwa mtu ambaye hajasaliwa kutoa mafunzo yanayohusu masuala ya kemikali, tunafahamu madhara ya kemikali na hivyo lazima wale ambao wanataka kutoa mafunzo tuwatambue kwa kuwasajili baada ya kujiridhisha,"amesema Ndiyo.

Wakati huo huo, Ndiyo amesema kuwa gharamza usajili umeshuka kutoka Sh.milioni moja hadi Sh.50,000 na hivyo ametoa rai kwa wananchi na hasa wanaojihusisha na biashara za kemikamili kwenda katika ofisi za mamlaka hiyo kwa ajili ya kusajiliwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Need some information about chemical permit for Transport.
    We transport some containers with engine oil. And port's agents ask for chemical permit.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...