Mashindano ya Taifa ya kuogoelea kwa waogeleaji wakubwa (Masters swimming championships) yatafanyika Jumamosi (Septemba 28) kwenye bwawa la kuogelea la shule ya Sekondari ya Shaaban Robert.

Mashindano hayo yatajumisha waogeleaji wenye umri kuanzia miaka 25 na zaidi yanatarajiwa kushirikisha waogeleaji mbalimbali wa mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha kuogelea Tanzania (TSA), Asham Hilal alisema jana kuwa mashindano hayo yamepangwa kuanza saa 2.00 asubuhi na kumalizika saa 11.00 jioni na leo ndiyo mwisho wa kuthibitisha.

Asmah alisema kuwa kila muogeleaji anatakiwa kulipa ada ya ushiriki kwa mujibu wa sheria ambapo waogeleaji ambao watafanya vyema watapata nafasi ya kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Kanda ya tatu hapo baadaye.

“Maandalizi yanaendelea vizuri na kuna mwitikio mkubwa kutoka kwa waogeleaji mbalimbali. Ni mashindano ya wazi ambapo mtu, au klabu zinaruhusiwa kushiriki,” alisema Asmah.

Alisema kuwa katika mashindano yaliyopita, klabu ya Taliss-IST illibuka katika nafasi ya kwanza. Mpaka sasa klabu hiyo imethibitisha kuwakilishwa na jumla ya waogeleaji 24 ambao kwa sasa po mazoezini chini ya kocha, Alexander Mwaipasi.

Alisema kuwa sheria za shirikisho la mchezo wa kuogelea duniani (Fina) zitatumika katika mashindano hayo ambapo waoegeaji wamegawanywa katika makundi ya miaka tofauti.

Makundi ya miaka hiyo ni 25 mpaka 29, 30 – 34, 35 – 39, 40 – 44, 45 – 49, 50 – 54, 55 – 59, 60 – 64, 65 – 69, 70 – 74, 75 – 79, 80 – 84, 85 – 89 na waogeaji wenye miaka kati ya 90 mpaka 94.

Mbali ya staili za butterfly, backstroke, Individual Medley, freestyle, breaststroke, waogeleaji pia watashindana katika ‘relay’ mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...