Na Woinde Shizza Michuzi Blog,Arusha

CHAMA cha Mawakala wa pembejeo za kilimo na mifugo mkoani Arusha kimeishauri Serikali kuwashirikisha katika mchakato wa upangaji wa bei elekezi za mbolea kwani ukubwa wa bei hizo unawapa changamoto kubwa wakati wa uuzaji.

Pia wameiomba Serikali kuangali namna ya kuwapunguzia bei za leseni na kodi ya mapato kwa kuwa biashara wanayoifanya ina sura ya kutoa huduma zaidi kuliko biashara.

Wakizungumza leo wanachama wa chama hicho wakati wa mkutano huo uliofanyika mkoani hapa wamesema lengo la kukutana kwao pamoa na mambo mengine watajadili rasimu ya Katiba ya chama hicho na kupatiwa vyeti vya mafunzo waliohitimu ya namna ya kutambua viatilifu feki na vizuri.

Kuhusu bei ya mbolea, Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala wa Pembejeo za Kilimo Mifugo wa Mkoa wa Arusha (ARAAFARMA) Titus Rweyumamu amesema bei kubwa za mbolea ambazo zinapangwa zinawaumiza wao kwani wateja wengi wao wengi ambao ni wakulima wanashindwa kuzimudu.

"Ingekuwa vizuri iwapo Serikali ingekuwa inatushirikisha katika mchakato wa upangaji wa be.Sisi ndio tunajua wateja wetu wapo maeneo gani na uwezo wao kiuchumi ili kumudu bei za pembejeo hizo za kilimo na mbolea.

"Ni imani yetu kuwa tutashirikiana vizuri na Serikali kufanikisha lengo la kuwa hudumia wakulima ili kufikia malengo yao ya uzalishaji wa mazao ya kilimo kwa kiwanago cha juu na hii inawezekana kabisa,"amesema .

Kwa upande wake Katibu wa Chama hicho Humphrey Mswia amesema wataendelea kushirikiana na Serikali nao ili waendelee kutoa huduma bora kwa wakulima wote.

Pia amesema lengo kubwa la kukutana ili kupita rasimu ya Katiba ya chama hicho ambacho kinafanya kazi ya kuwaleta pamoja mawakala wote wa pembejeo mkoani Arusha kwa lengo la kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria za nchi.

"Mkakati wetu ni kutoa huduma bora kwa wakulima ili kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo pamoja na kufanikisha kauli mbiu ya Serikali ya viwanda. Tunafahamu kilimo ndicho kitakachotoa malighafi kwa ajili ya viwanda vyetu,"amesema.

Ameongeza kuwa wataendelea kufanya utafiti wa matumizi bora ya pembejeo, dawa na Masoko.Pia kufanya utetezi na ushawishi kwa wakulima mawakala wa pembejeo za kilimo na mifugo kutoa elimu ya kuhifadhi na kuendeleza mazingira kwa wanachama najamii nzima kwa ujumla. 

Wakati huo huo mgeni rasmi wa mkutano huo ambaye ni Ofisa Mipango Mkoa wa Arusha Moses Mabula amesema Serikali itashirikiana nao bega kwa bega kuhakikisha wanawapa huduma bora wakulima na wafugaji.

Amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi wake wanapata elimu ya matumizi sahihi ya pembejeo za kilimo.Aidha amewaahidi wanachama hao kuwatafutia wataalamu ambao watawapa elimu na mafunzo ili nao wawaelimishe wakulima.

Pia amesema itaendelea kutafuta ufumbuzi wa changamoto ambazo zimeanishwa na chama hicho.
 Afisa mipango ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha Moses Mabula akitoa nasaaha zake mara baada ya kuwafungulia mkutano wao 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...