MFUKO wa ubunifu kwa maendeleo ya watu  (HDIF) umesema utaendelea kushirikiana  na serikali katika kuwanyanyua wabunifu nchini ili kuwapa nguvu katika kazi zao za ubunifu.

 Mkurugenzi mkaazi wa HDIF, Joseph Manirakiza, ameyasema hayo Mjini Dodoma wakati akizungumza na wadau mbalimbali kutoka serikalini pamoja na taasisi zisizo za kiserikali katika warsha ya ubunifu iliyoandaliwa na HDIF kwa ushirikiano wa COSTECH na baraza la Taifa la uwezeshaji NEEC.

Amesema, tangu kuanzishwa kwa mfuko huo mwaka 2014, Jumla ya miradi 43, imeishasaidiwa.

“Lengo ni kuhakikisha tunashirikiana na serikali katika kuwanyanyua wabunifu, zipo sekta nyingi ambazo zinatuhusu ili kuweza kushirikiana nayo,” alisema Manirakiza.

Kwa upande wake mkurugenzi wa tume ya sayansi na teknolojia (Costech), Dk. Amos Nungu amesema serikali imeamua kukutanisha wadau kutoka wizara nne tofauti ili kuweza kujadiliana na kuzungumzia sera.

Dk. Nungu alisema, “wadau wa sekta hizo wanakutanishwa pamoja kwa lengo la kujadiliana na kuzungumzia sera, kwani ni mara ya kwanza tangu kukutana.”

 Naye mwakilishi wa baraza taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC) Gwakisa Bapala, alisema wao ni wadau ambao wanashirikiana na HDIF ili kuwawezesha na kuwainua wananchi kiuchumi.

Akizungumzia mafanikio ya mfuko huo, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mh. Godwin Gondwe, alisema kupitia mradi wa HDIF wilaya yake imefanikiwa kujenga zaidi ya vyoo 20 vya ubunifu.

“Vyoo ambavyo vinajengwa wilayani kwangu kupitia mfuko huo, vinabana matumizi ya maji kwani maji yanayotumika ni kidogo na mtu anakuwa msafi….hii ni mojawapo ya ubunifu mkubwa uliofanywa wilayani kwetu,” alisema Mh. Gondwe.

 Mtaalamu wa mawasiliano wa Human Development Innovation Fund ( HDIF) bi Hannah Mwandoloma akikaribisha washiriki wa warsha ya ubunifu iliyoandaliwa na HDIF kwaushirikiano wa COSTECH  Na Baraza la Taifa la uwezeshaji NEEC.
 Mkurugenzi Mkazi wa HDIF Be Joseph Manirakiza akitoa mada juu ya ubunifu katika warsha ya ubunifu iliyoandaliwa na HDIF kwaushirikiano wa COSTECH  Na Baraza la Taifa la uwezeshaji NEEC
 Mkurugenzi wa COSTECH Dr. Amos MUNGU akifungua warsha ya ubunifu iliyoandaliwa na Mfuko wa Ubunifu kwa Maendeleo ya Watu (HDIF) kwa ushirikiano wa COSTECH  Na Baraza la Taifa la uwezeshaji NEEC.
 Mkuubwa wilaya ya Handeni Be Godwin Gondwe akiwasilisha mada katika warsha ya ubunifu iliyoandaliwa na Mfuko wa Ubunifu kwa Maendeleo ya Watu (HDIF) kwa ushirikiano wa COSTECH  Na Baraza la Taifa la uwezeshaji NEEC.
 Mwanzilishi na mkurugenzi wa shirika la Shule Direct Bi.Faraja Nyalandu akielezea jinsi ubunifu wa shirika lake lilivyo saidia wanafunzi na walimu was Tanzania katika warsha ya ubunifu iliyoandaliwa na Mfuko wa Ubunifu kwa Maendeleo ya Watu (HDIF) kwa ushirikiano wa COSTECH  Na Baraza la Taifa la uwezeshaji NEEC.
 Washiriki wakifuatilia madabzilitolewa na wawasilishaji katika Mkurugenzi wa COSTECH Dr. Amos MUNGU akifungua warsha ya siku moja ya ubunifu iliyoandaliwa na Mfuko wa Ubunifu kwa Maendeleo ya Watu (HDIF) kwa ushirikiano wa COSTECH  Na Baraza la Taifa la uwezeshaji NEEC.
 Mtaalamu wa mawasiliano akiwasilisha Jambo kwa washiriki wa warsha ya ubunifu iliyoandaliwa na HDIF kwaushirikiano wa COSTECH  Na Baraza la Taifa la uwezeshaji NEEC.
 Mkurugenzi wa COSTECH Dr. Amos MUNGU akifungua warsha ya ubunifu iliyoandaliwa na Mfuko wa Ubunifu kwa Maendeleo ya Watu (HDIF) kwa ushirikiano wa COSTECH  Na Baraza la Taifa la uwezeshaji NEEC
Washiriki toka wizara mbali mbali na taasisi za serikali pamoja na baadhi ya wagunduzi wa miradi iliyofadhiliwa na HDIF Wakisikiliza mada katika warsha ya ubunifu iliyoandaliwa na Mfuko wa Ubunifu kwa Maendeleo ya Watu (HDIF) kwa ushirikiano wa COSTECH  Na Baraza la Taifa la uwezeshaji NEEC

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...