Na Said Mwishehe,Michuzi TV

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt .John Pombe Magufuli ametoa siku saba kwa watuhumiwa wa kesi za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha ambao wako mabuhusu kukubali makosa yao na kuahidi kutorudia tena ili watolewe mahabusu ambako wamekaa kwa muda mrefu.

Pia amesema baada ya kukubali makosa walipe fedha zikiwemo walizohujumu,utakatishaji,kukwepa kodi ya Serikali na aina nyingine ya hujuma, na watakaoshindwa kukubali ndani ya muda huo ambao ameutoa basi watabaki huko huko mahabusu ili sheria uendelee kuchukua mkondo wake.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Septemba 22,2019 Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa kuwapisha viongozi mbalimbali aliowateua juzi akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ambapo baada ya kuapisha viongozi hao ametumia nafasi hiyo kuonesha kusikitsha kwake na mahabusu waliokaa muda mrefu ambao wengine wanatuhumiwa kwa kesi za utakatishaji fedha na uhujumu uchumi.

"Kwa kweli naumia sana moyo ninapoona mahubusu wanakwenda mahakamani na kurudi mahabusu ,wengine wamekonda.Najua haya mambo yanakwenda kwa mujibu wa sheria,ingekuwa uwezo wangu ningewasamehe wote wenye kesi za aina hiyo baada ya kukubali makosa na kuahidi kutorudia tena.

"Mimi natoa wazo tu,wanasheria mtaangalia kama inawezekana,binafsi napenda waondolewe mahabusu,natamani kuona mahabusu wanapungua na ikiwezekana siku moja niamke na kukuta hakuna mahabusu magerezani,'amesema Rais Magufuli.

Ametumia nafasi hiyo kutoa ushauri kwa DPP pamoja na wakuu wengine wa Idara zinazohusiana na mahabusu kukaa na ndani ya siku saba wale wote ambao watakiri makosa wawekewe utaratibu wa kulipa fedha."Natoa siku saba kuanzia leo".

"Kwani leo siku gani. Ni Jumapili,kumbe ni siku nzuri sasa kuanzisha kesho mkae DPP na wenzako kwa ajili ya kushughulikia hili.Huu ni ushauri wangu kwenu,niliwahi kusema huko nyuma sitaki kuongeza nchi ambayo watu wake wametawaliwa na machozi,"amesema.

Wakati anazungumzia kupunguzwa kwa mahabusu Rais Magufuli amesema Mkuu wa Magereza nchini , amemuandikia barua kwa ajili ya kuomba kuongeza askari magareza ambapo wanahitaji askari magereza 800."Nimeiangalia ile barua sijajibu na ukweli siwezi kukubali ombi lao. Badala ya kufikiria kupunguza mahabusu wanafikiria kuongeza askari."

Wakati huo huo Rais Magufuli amezungumzia suala la kuteua na kutengua teuzi ambako amesema ni kazi ngumu inayomuumiza kichwa na wala hayaendi kutengua lakini kuna wakati anavumilia mambo yanavyokwenda lakini ameamua kutengua na hasa ninapoona aliyepewa nafasi nashindwa kutimiza wajibu wake.

"Viongozi wenzangu kafanyeni kazi,sipendi kutengua lakini inabidi.Unakwenda kwenye Mkoa unakuta mambo hayaendi,tupo kwa ajili ya kuwatumikia hawa wananchi masikini. Kuna siku nitateungua kuanzia Mkuu wa Mkoa hadi Mtendaji wa kijiji tena kwa siku moja na kuteua wengine,"amesema Rais Magufuli na kusisitiza sio kwamba anawatisha lakini yeye anahimiza kufanya kazi kwa bidii.
Rais  Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kuwaapisha Viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...