Charles James, Michuzi TV

SERIKAL imesema kuna haja ya kuwa na tafiti nyingi za afya ambazo zitasaidia kujua sekta hiyo inakabiliwa na changamoto zip ili ziweze kutatuliwa kwa haraka na ufanisii.

Akizungumza leo jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Huduma za Afya na Ustawi wa Jamii TAMISEMI, Dk Ntuli Kapologwe amesema ni vema kama Serikali wafanye tafiti ili kurahisisha utendaji kazi katika mfumo wa Afya nchini.

Dk Kapologwe ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa tathimini ya miradi ya afya ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Mzumbe.

“Wakati tukielekea katika uchumi wa kati ifikapo 2025 ni lazima tuhakikishe sekta ya afya inakuwa vizuri,na tunajua mfumo wa afya umekaa kama ‘Pyramid’ tunataka huduma bora zianzie kuanzia anapoingia katika hospital apate huduma nzuri,”amesema.

Kapologwe amesema kuna umuhimu wa kupata tafiti nyingi ambazo zitaisaidia sekta ya afya kujua kuna tatizo gani na kuweza kuyatatua kwa wakati hivyo kumsaidia mwananchi wa chini ambaye siku zote ndio kimbilio.

Aidha,amesema kuna haja ya tafiti hizo ziunganishe sera na utekelezaji huku akitaka zishiishie tu kwenye machapisho bali zifike kwa wahusika na kutekelezwa.

“Tafiti zisiishie tu kwenye machapisho,sisi kama wizara tunataka tafiti nyingi ambazo zitatusaidia katika utendaji kazi wetu,. Mfano sasa hivi tumejenga majengo mengi tunataka tafiti Je,huduma kwa sasa zipoje,? Je huduma ni bora? Amesema Dk Kapologwe.

Dk Kapologwe amesema kuwa kipimo cha utendaji kazi kwa sasa kipo kwa mwananchi kwa kuhakikisha anapata mahitaji yake yote ambayo ni muhimu.Aidha amevitaka vyuo vikuu nchini kushirikiana na Ofisi za Mkuu wa Mkoa na Wilaya ili kuweza kushughulikia changamoto na kuzitambua ndani ya kipindi cha muda mfupi.

Nae Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Prof Ganka Nyamsongoro amesema kuwa watanzania wanapaswa kujijengea utamaduni wa kutumia takwimu ili kupata tija katika kazi zao.
Mkurugenzi wa Afya na Ustawi wa Jamii TAMISEMI, DK Ntuli Kapologwe akizungumza katika uzinduzi wa mkutano wa tathimini ya miradi uliondaliwa na Chuo Kikuu cha Mzumbe Jijini Dodoma leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...