Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Afya wa Marekani Admiral Brett Giroir. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ubalozi wa kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulioko New York Marekani.



Katika kufikia azma ya kuwa na uchumi jumuishi Tanzania iko katika utekelezaji wa mkakati mpya wa matumizi ya fedha kwa mfumo usio wa kibenki ambao umewalenga wakulima wadogo na wakati hususani wanawake ili kuleta usawa wa kijinsia Nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi wakati akizungumza kwenye mkutano wa viongozi wa juu kuhusu masuala ya uchumi jumuishi kwa maendeleo uliondaliwa kwa pamoja na Tazania na Uholanzi.

Akizungumza katika Mkutano huo, kando ya mkutano wa 74 wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa unaoendelea New York MarekaniProf. Kabudi ameelezea mafanikio ambayo Tanzania imefikia katika mpango wake wa kwanza kuongeza watu katika mfumo wa fedha usio wa kibenki na sasa iko katika mpango wa pili ambapo watumiaji wa mfumo wa fedha usio wa kibenki wameongezeka maradufu.

Aidha ameongeza kuwa matumizi ya kidijitali katika kutoa huduma za kilimo,kutafuta masoko ya bidhaa pamoja na kuwawezesha wananchi kupata fedha ikiwa ni pamoja na vicoba kwa kiasi kikubwa imeongeza pia idadi ya wanawake katika kuleta usawa wa kijinsia.

Kwa upande wake Balozi na mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Malkia Maxima amesema kwa kiasi kikubwa anaridhishwa na hatua ambazo Tanzania inazichukua kwa nia ya kupunguza umasikini,na kutengeneza ajira na kuleta usawa wa kijinsia kwa kuwawezesha wananchi wake kuwa na njia ya kujiongezea kipato kupitia mfumo wa kifedha usio wa kibenki.

Malkia Maxima amezisisitiza serikali na sekta binafsi kuona umuhimu wa kuongeza upatikanaji wa huduma kupitia mfumo wa fedha usio wa kibenki hususani kwa wakulima ili tija ionekane zaidi kwa wananchi hususani kwa wakulima wa kipato cha chini na kati.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...