Kamanda wa polisi mkoani Arusha, Jonathan Shana katika matukio mbalimbali.

Jeshi LA Polisi  Arusha,linawashikilia vibaka hatari wa kundi la tatu mzuka wapatao 13 ambao wamekuwa wakijihusisha na matukio ya uporaji, unyang'anyi na wizi wa kutumia nguvu huku wakiwalenga zaidi wanawake.

Kamanda wa polisi mkoani Arusha, Jonathan Shana amewataja vinara watatu kati ya 12 ambao wakuwa wakiongoza kundi hilo kuwa ni Faisal Mbaraka(17),Emmanuel Bosco(20) na Mohamed Hussein (18)wote wakazi wa Sanawari jijini hapa.

Kamanda Shana ametaja vitu hivyo kuwa ni pamoja na Pikipiki nne ,MC 504AHT aina ya Kinglion,MC262AXQ aina ya Boxer ,MC240AEB aina ya Boxer na MC 811BWG aina ya Haojue.

Vitu vingine ni Laptop tatu,TV kubwa tatu,Meza mbili za TV Friji moja aina ya Boss na Redio kubwa moja ikiwa na spika zake mbili aina ya Sonny vikiwa vinashikiliwa kituoni hapo.

Kamanda wa Polisi amewataka wananchi walioibiwa vitu vyao kufika kituoni hapo na kuvitambua.

Picha ikionyesha Kamanda Wa Polisi akionyesha baadhi ya vitu bilivyokutwa na vibaka hao

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...