MKUU wa wilaya Kigamboni Sarah Msafiri amewataka vijana wa wilaya hiyo kujitokeza kugombea kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa huku akiwaeleza kuwa uchaguzi huo si wakuunda Serikali bali ni wa kumsaidia majukumu Dkt John Magufuli .

Amesema kuwa Serikali tayari ipo Madarakani ambayo imetokana na Chama cha Mapinduzi CCM hivyo nivema wakajitokeza kugombea na si kuwaachia akina Baba tu.

Sarah ameyasema hayo jana Wilayani humo wakati akizungumza na wananchi wa tarafa ya Somangila kuhusu kuchangamkia fursa mbalimbali zinazojitokeza kupitia Manispaa hiyo ya Kigamboni .Amewaeleza kuwa mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi wa Serikali za Mtaa hivyo vijana ,na akinamama wajitokeze kugombea ili kuweza kupata nafasi za uongozi .

Kuhusu fidia kwa baadhi ya Wananchi kupitia mradi wa Temeke Sarah alisema mwenzi octoba mwaka huu Waziri wa Ardhi William Lukuvi atakuja kuzungumzia fidia hiyo.
Amesema anatambua kuwa kuna wananchi ambao walitakiwa wapatiwe fidia kutokana na maeneo yao kuchukuliwa na Serikali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi.mbalimbali hivyo Waziri Lukuvu atakuja kutolea ufafanuzi

Akizungumzia fursa za mikopo Wilayani humo Sarah alisema Manispaa imejipanga kikamilifu kutoa fursa za mikopo nakwamba Serikali imeshatoa shilingi bilioni 10 kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vijana na akina mama.Amesema mikopo hiyo ipo na Mwezi ujao wataaza kutoa mikopo hiyo hususani kwa wale wenye vigenzo na mikopo hiyo itakuwa na riba nafuu sana kulingana na kiwango cha Fedha atakachochukuwa.ambapo hautazidi shilingi 2000.

Pia Mkuu wa wilaya Sarah akizungumzia Miundombinu ya barabara amesema Serikali inatambua changamoto hiyo na mpango kabambe upo tayari kwa ajili kutengeneza barabara.Amesema kuwa Serikali ya Wilaya nimeshaweka mpango mkakati wa muda mfupi ili kuweza kutatua sehemu ya changamoto za barabara hizo ili kuepusha kujitokeza kwa Mafuriko kama ilivyo sasa.

Pia Sarah amewaeleza wananchi hao kuwa Wilaya imetenga hekari nne kwa ajili ya Wananchi kufanya biashara mbalimbali wakiwamo mama lishe,wauza vinywaji baridi ambavyo si vileo hivyo wajitokeze kupeleka Maombi yao ili kuweza kupata nafasi hiyo.

Kwaupande wake Mkuu wa kituo cha Polisi Wilaya ya Kigamboni OCD John Makuri aliwataka wananchi kuendelea kulinda amani hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa Serikali ya mitaa.

Amesema nivema wakajiepusha ma masuala ya uovu na badala yake waendelea kudumisha ,kulinda amani iliyopo na kwamba yeyote atakayejihusisha na vitendo viovu hatua Kali dhidi yake zitachukuliwa.
Mkuu wa Wilaya Kigamboni,Sarah Msafiri akizungumza na wananchi wa Tarafa ya Somangila leo kuhusu vijana kujitokeza kugombea kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa.hayo yalizungumzwa na Mkuu wa Wilaya katika ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi,kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Mrakibu Mwandamizi wa Polisi,John Makuri akizungumaza leo na wananchi wa Tarafa ya Somangila Wilaya ya Kigamboni kuhusu kuendelea kulinda amani hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa Serikali ya mitaa.
Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Rahel Muhando akizungumza wakati akizungumza wakati alipokuwa akitambulisha sehemu ya viongozi wa ngazi mbalimbali wa Wilaya hiyo katika mkutano wa Mkuu wa Wilaya hiyo wa kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi,kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...