WAFANYAKAZI wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam jana walijitolea kufanya usafi katika Hospitali ya Amana ya jijini Dar es Salaam pamoja na kukabidhi vifaa mbalimbali vya kufanyia usafi, ikiwa ni kuadhimisha siku ya usafi duniani zilizofanyika Septemba 21, 2019.

Akizungumza na wanahabari mara baada ya zoezi hilo katika Hospitali ya Amana, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Bw. Badru Idd alisema zoezi hilo ni utaratibu wa kawaida ambao NMB imejiwekea kuona ni jinsi gani inarudisha sehemu kidogo ya mapato yake katika jamii.

Alisema mbali na zoezi la kufanya usafi hospitalini hapo, wafanyakazi hao walikabidhi vifaa tofauti vya kufanyia usafi vikiwemo vifaa vya kuzolea na kuhifadhia taka, mifagio, vifaa vya kudekia, seti za vifaa vya kujikinga wakati wa kufanya usafi, buti za kufanyia usafi, makoleo maalum ya taka na dawa za usafi.

"...Leo tumekuja Hospitali ya Amana kwa ajili ya kujitolea kufanya usafi kuitikia maadhimisho ya usafi duniani, tumejipanga kufanya usafi maeneo mbalimbali ya nchi kwa kuwa tuna mtandao mpana vivyo hivyo wenzetu maeneo mbalimbali wanafanya usafi kama sisi. Na sisi kama kanda ya Dar es Salaam tumeamua kuja kufanya usafi Hospitali ya Amana."

Akifafanua zaidi alisema NMB pia imekuwa ikitumia fungu hilo katika kusaidia jamii kwenye elimu, afya pamoja na majanga pale yanapojitokeza kwa jamii yetu. "Hii yote ni kuleta ukaribu wa Benki yetu na jamii...hatuji tu kuomba biashara kwa jamii bali tunajitokeza kushiriki, na kusaidiana na jamii katika kufanya shughuli zao. Vifaa vyote tulivyokabidhi leo ni fedha zilizochangwa na wafanyakazi wetu kwa hiyari kujitolea kusaidia jamii," alisema Bw. Idd.

Aidha aliongeza kuwa NMB wakati wote imekuwa ikishirikiana na jamii katika shughuli mbalimbali, ikiwemo kutenga asilimia moja ya pato lake baada ya kuondoa gharama zote, na kwa mwaka huu imetenga zaidi ya bilioni moja kwa aajili ya shughuli za kijamii, huku hadi kufikia mwezi Julai, 2019 NMB imekwishatumia zaidi ya milioni 450 kwa shughuli kama hizo.

Ofisa Muuguzi Kiongozi wa Hospitali ya Amana, Vicent Semkamba (kulia) akipokea sehemu ya vifaa vya kufanyia usafi kutoka kwa mmoja wa maofisa wa Benki ya NMB jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni msaada uliotolewa na wafanyakazi wa benki hiyo walipojitolea kufanya usafi katika hospitali hiyo.
Mmoja wa maofisa wa Benki ya NMB jijini Dar es Salaam akifyeka majani kwa kutumia mashine maalum Hospitali ya Amana walipojitolea kufanya usafi katika hospitali hiyo.
Sehemu ya wafanyakazi wa Benki ya NMB jijini Dar es Salaam wakifanya usafi maeneo mbalimbali ya Hospitali ya Amana leo ikiwa ni kujitoa kushiriki matendo ya kusaidia jamii.
Sehemu ya wafanyakazi wa Benki ya NMB jijini Dar es Salaam wakifanya usafi maeneo mbalimbali ya Hospitali ya Amana leo ikiwa ni kujitoa kushiriki matendo ya kusaidia jamii.
Ofisa Afya Hospitali ya Amana, Avit Maro (kulia) akiwashukuru wafanyakazi wa Benki ya NMB mara baada ya zoezi la kufanya usafi katika hospitali hiyo. Katikati ni Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Bw. Badru Idd.

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Bw. Badru Idd (kushoto) akitoa maelekezo kwa wafanyakazi wa benki hiyo kabla ya kuanza kufanya usafi katika Hospitali ya Amana walipojitolea. Mbali na kujitolea kufanya usafi wafanyakazi hao pia walikabidhi vifaa mbalimbali vya kufanyia usafi hospitalini hapo.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Bw. Badru Idd (kulia) akimkabidhi sehemu ya vifaa vya kufanyia usafi Ofisa Muuguzi Kiongozi wa Hospitali ya Amana, Vicent Semkamba (kushoto) ikiwa ni msaada uliotolewa na wafanyakazi wa benki hiyo walipojitolea kufanya usafi katika hospitali hiyo. Mbali na kujitolea kufanya usafi wafanyakazi hao pia walikabidhi vifaa mbalimbali vya kufanyia usafi hospitalini hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...