Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.Kangi Lugola akizungumza mara baada ya kukabidhiwa rasmi uwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa nchi wanachama wa majeshi ya Polisi za nchi za ukanda wa mwa Afrika(EAPCCO) katika kikao cha 19 cha baraza la mawaziri kilichofanyika Jijini Arusha

Na.Vero Ignatus,Arusha.


Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.Kangi Lugola amekabidhiwa rasmi uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa nchi  wanachama wa majeshi ya Polisi za nchi za ukanda wa mwa Afrika(EAPCCO) katika kikao cha 19 kilichofanyika Jijini Arusha leo sep20 kutoka kwa Waziri wa mambo ya ndani wa nchi ya Sudani ambapo amewakilishwa na Luteni Jeneral wa Polisi Adil Mohamed


Akizungumza baada ya kukabidhiwa uwenyekiti Waziri Lugola amesema kuwa anaahidi kufanyia kazi na kuzingatia maagizo yote yanayotakiwa kutekelezwa na kuendeleza  mafanikio ya kuondoa changamoto zinazokabili ukanda wa Afrika.


Amesema kuwa yapo makubaliano ya msingi ambayo wamekubaliana katika mkutano ambayo yanazitaka nchi wanachama kupitia EAPCCO kuendelea kujipanga kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka kama vile ugaidi,utakatishaji wa fedha haramu,wizi wa magari,biashara haramu ya dawa za kulevya,usafirishaji wa binadamu,uuzaji na usafirishaji wa silaha uhalifu wa ujangili na uharamia,pamoja,uhalifu mwingine.


Amewahakikishia wananchi wa nchi zote hizo 14 kuwa msingi mkubwa wa ustawi wa maisha ni msingi mkubwa wa maendeleo ya wanadamu ikiwa ni pamoja na maisha ya wananchi na mali wanahitaji kuhakikishiwa ulinzi na majeshi hayo ya polisi katika nchi wanachama.

Katibu mtendaji wa Interpol Jurgen Stock amesema wao wataendelea kutoa ushirikiano na kuangalia namna ambavyo watapambana na uhalifu wa kimtandao na ugaidi haswa katika ukanda wa Mashariki sambamba na kupambana na rushwa na uhalifu unaovuka mipaka.


Amesema kuwa Mfumo wa mawasiliano umeweza kuwagharimu zaidi dola mil 99 kwaajili ya kuangalia nini kinachoendelea katika nchi za ukanda wa Mashariki na namna tunavyoweza kufanya kazi pamoja na kuhakikisha kuwa tunakuwa na mfumo wa kutoa taarifa kwa pamoja .Stock amesema kuwa ushirikiano unahitajika katika nyanja zote ikiwemo mafunzo ya watendaji,haswa mafunzo maalum ,makosa yanavyovuka mipaka ,operesheni za pamoja kufanya upelelezi wanpamoja wa kubaini taarifa za kiitelijensia.Akisoma risala ya kufunga kikao hicho cha Mawaziri  wa EAPCCO Lugola amelishukuru Baraza hilo la Mawaziri kwa kumuamini na kumchagua kuwa mwenyekiti kwa mwaka 2019-2020 amewaomba nchi wananchama kuendeleza ushirikiano sambamba na kuwa na utashi wa kusiasa.Amesema kuwa katika ukanda wa mashariki kuna changanoto mbalimbali za uhalifu,maeneo ya msingi ni kuwajengea watendaji wao uwezo huku akiwataka viongozi wa Askari kuimarisha nidhamu kazini sambamba na kuepuka visingizio.MWISHO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...