Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akizungumza na wavuvi leo 29/9/2019 katika bwawa la Nyumba ya Mungu wilayani mwanga Mkoani Kilimanjaro.

Zana zinazo tumika katika shughuli za Uvuvi Haramu zenye Thamani ya zaidi ya million 150, ikiwemo vyavu aina kokoro 56, kwa lengo la kupiga Vita Uvuvi haramu zikiteketezwa kwa Moto leo katika bwawa la Nymba ya Mungu Kilimanjaro.



Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akisisitiza jambo kwa wavuvi pamoja na wananchi waliojitokeza kumsikiliza leo katika eneo la Bwawa la nyumba ya Mungu Mwanga Kilimanjaro.


NA:Vero Ignatus,Mwanga Kilimanjaro.


Serikali imeteketeza kwa Moto zana zinazo tumika katika shughuli za Uvuvi Haramu zenye Thamani ya zaidi ya million 150, ikiwemo vyavu aina kokoro 56, kwa lengo la kupiga Vita Uvuvi haramu katika bwawa la Nyumba ya Mungu wilayani mwanga Mkoani Kilimanjaro.

Akiwa katika Oparesheni maalumu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina amesema serikali itaendelea kupiga Vita Uvuvi haramu kwa ajili ya kunusuru mazalia ya viumbe hai wa majini kwa maslahi ya vizazi vijavyo.

Waziri Mpina amewataka wale wote wanaojishughulisha na uvuvi haramu katika Bwawa la Nyumba ya Mungu ambapo uvuvi haramu umeshamiri kuacha mara moja ambapo zoezi hilo la kuwasaka wavuvi haramu liakuwa la nchi nzima

''Hivi sasa tunachoma nyavu hapa za ni safari tuliyoianza ya kuchoma nyavu na kukamata wavuvi haramu, na wale wote wanaojishughulisha na uvuvi haramu nchi nzima ,kwahiyo tunaanza safari hapa mwanga ambapo safari hii itakuwa ni ya nchi nzima "Alisema Mpina

Katika Hatua nyengine Waziri Mpina ametoa miezi mitatu kwa halmashauri ya wilaya ya mwanga kuhakikisha Ujenzi wa choo Bora kwa ajili ya wavuvi na Wafanyakazi Biashara wa eneo hilo vinginevyo Marufuku halmashauri kukusanya ushuru katika eneo Hilo.

"Halmashauri inaendelea kukusanya mapatao kila uchao na wala hawachoki hawana likizo wala jumapili,lakini choo tu wakati mwingine hata milioni mbili hakifiki,kimeshindikana kujengwa,ifikapo tarehe 30/12/2019nitarudi hapa kuja kukagua,nikikuta hakuna mwalo,nikikuta hakuna vyoo,nitaifungia halmashauri ya mwanga kukusanya chochote"akisema Mpina

Samuel Kifoyo ni Mkazi wa mwanga ambae imeelezwa amekuwa akitafutwa na Baadhi ya watu wakiwemo Baadhi ya Askari kwa tuhuma mbalimbali ambapo baada ya kupata taarifa za ujio wa waziri wa uvuvi anajitokeza adharani akiwa katika mavazi ya kike kuhofia kupigwa na mahasimu wake Katika kata ya Lang'ata Kama anavyo anabainisha.

"Nimekuja hapa leo ili unilinde ,mama yangu ni mjane kazi yake anakata kuni nimeteseka nimekaa muda mrefu,watu wametoa pesa ili nikamatwe niuliwe na dada huyo yupo hapa,na leo alikuwa aseme kama alivyosema mwanga ndiyo maana nikaona bora mimi nikaona niwahi,nilikuwa nimejificha kwenye mapori nikivizia msafara wako mheshimiwa".Alisema Samweli Mkazi wa Mwanga.

Joachim Haule na Juma Waziri ni Baadhi ya wakazi wa kata hiyo wanasema eneo Hilo bado Hali ya usalama si shwari na hapa wakaeleza changamoto wanazo kabiliana nazo katika Oparesheni zinazo fanywa eneo Hilo.

Kwa mujibu wa wizara ya mifugo na uvuvi kwa sasa tanzania inasamaki wakutosha bila kuagiza nchi nyengine lakini bado suala la Uvuvi haramu limeshamiri katika Baadhi ya maeneo Kwenye maziwa na baharini, huku Oparesheni zilizo kuwa zikiendelea miaka iliyo pita zikianza upya kwa Kasi kubwa maeneo yote ya uvuvi na mifugo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...