Na, Editha Edward, Globu ya Jamii - Tabora 

Askari polisi sita wa kituo cha polisi Igunga pamoja na Mwenyekiti wa kitongoji cha Isakamaliwa wanatarajiwa kufikishwa mahakamani na Taasisi ya kupambana na Rushwa TAKUKURU  mkoani Tabora kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa zaidi ya Shilingi milioni nane na laki nne kwa wananchi wawili ili wasiwafikishe kwenye vyombo vya sheria 

Kwa mujibu wa kaimu mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Tabora Mussa Chaulo amesema Askari hao wote sita kwa kushirikiana  na viongozi hao wawili wa serikali ya kijiji hicho cha Isakamaliwa kwa pamoja walishirikiana kuomba na kupokea rushwa hiyo kwa wananchi wawili akiwemo mzee mwenye umri wa miaka 95 ili wasiwafikishe kwenye vyombo vya sheria wakiwatuhumu kwa kujihusisha na Imani za kishirikina na kumiliki silaha ya moto pamoja na kukutwa na madawa ya kulevya aina ya bangi
Kaimu Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Tabora, Mussa Chaulo
Katika mwendelezo wa jitihada hizo za kupambana na rushwa taasisi hiyo imefuatilia miradi 14 ya maendeleo katika kipindi cha mwezi julai hadi septemba 2019 yenye thamani ya Shilingi bilioni moja milioni thelathini na nne laki saba tisini na nane elfu miambili sabini na tisa katika Sekta za afya, elimu, maji na Ujenzi wa masoko ambapo ufuatiliaji wa miradi hiyo ulibaini kuwepo na viashiria vya ukiukwaji kwa utaratibu kwenye utekelezaji wa mradi mmoja wa Ujenzi wa soko hivyo imeanzisha uchunguzi kuona kama kuna vitendo vya rushwa katika mradi huo

Aidha taasisi hiyo ya kupambana na rushwa imeendelea kusisitiza kuwa imejipanga vyema kuwashughulikia wale wote watakao jihusisha na vitendo vya rushwa katika Uchaguzi wa serikali za mitaa na hata utendaji Mzima wa Shughuli za uma

"hatuta mvumilia mtu yeyote atakae jihusisha na vitendo vya rushwa hatua sitahiki za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakae jihusisha katika Uchaguzi ni fursa tunayopata kwa ajili ya kuwachagua viongozi, wananchi tutumie fursa hii ya Uchaguzi kuchagua viongozi waadilifu "Amesema Chaulo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...