MKUU wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Edward Mpogolo amewata wananchi wa Wilaya hiyo kutumia muda uliobaki kujiandikisha katika daftari la uchaguzi wa serikali za mitaa ili waweze kutumia haki yao kuchagua viongozi.

Mpogolo alisema hayo  leo alipozungumza na waandishi wa habari katika Kitongoji cha Mtakuja, Kijiji cha Ikungi katika Wilaya hiyo alipokwenda kujiandikisha, aliwataka wananchi wa Ikungi kutumia haki yao ya Kidemokrasia ya kuchagua na kuchakuliwa. 

Aidha amesema uchaguzi ngazi wa serikali ngazi ya Vitongoji na Vijiji ni muhimu wananchi hushiriki moja kwa moja kupanga na kuamua kutekeleza maendeleo yao. 

"Hivyo ni muhimu kwa kila mwana Ikungi kushiriki kwakuwa inaamua hatima yake ya kujiletea maendeleo ambayo Rais John Magufuli amekuwa akipambana kwa watanzania. 

Alisema hadi jana wameandikikura.zaidi ya asilimia 41  ambapo wameweka mikakati kuhakikisha wanafikia lengo la kuandikisha watu 154137.

Mpogolo aliwahimiza wananchi aliowakuta katika kituo hicho  pamoja na vituo vingine alivyotembelea kuwahimiza vijana wao ambao umri wao ni juu ya miaka 18 kuhakikisha nao wanajiandikisha ili waweze kupata nafasi ya kuchagua viongozi ambao watawaletea maendeleo.

"Wazee wangu, tuwahimize na vijana wetu nyumbani nao wajiandikishe tusikubali wakabaki bila kujiandikisha nafasi hii ni muhimu kuitumia ili nao wawe sehemu ya kuchagua viongozi wanaowataka," alisema Mpogolo.

Aidha, alisema maendeleo katika nchi hayawezi kushuka kutoka Mbinguni bali kwa kuchagua viongozi imara, wenye mapenzi na maendeleo ya wananchi na pia maendeleo ya nchi yao.

Mpogolo alitembelea vituo vingine katika Wilaya hiyo ambapo alizungumza na wananchi kujua changamoto zao katika uandikishaji huo na pia kuwahamasisha kuwashauri na watu wengine kujitokeza.

"Msiwaache watu nyumbani tuhakikishe wote wanajiandikisha, kina mama nyumbani, majirani," alisema. 

Mpogolo alisema katika Wilaya hiyo uandikishaji unaenda vizuri, watu wanajitahidi kujitokeza na pia viongozi wanajitahidi kuhamasisha wananchi kujitokeza ili kuhakikisha kila mmoja anashiriki kupiga kura.
MKUU wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Edward Mpogolo akijiandikisha  katika daftari la uchaguzi wa serikali za mitaa,katika Kitongoji cha Mtakuja, Kijiji cha Ikungi Wilayani humo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...