Na, Editha Edward-Tabora 

Baadhi ya Wasichana Mkoani Tabora wamesema hawata kuwa nyuma kuwania nafasi za uongozi katika chaguzi za Serikali za Mitaa na Uchaguzi mkuu ujao wakiamini Kuwa kupata uongozi kutasaidia kuimarisha nguvu Katika Kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyodaiwa kuja ndoto za maisha yao

Wameyasema hayo katika kongamano la ajenda ya msichana ya 2019 lililoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Msichana Initiative lililofanyika chuo cha utumishi wa Uma mjini Tabora ambapo limehusisha  wasichana 800 kutoka katika wilaya tatu za mkoa wa Tabora ambazo ni Uyui, Nzega, na Tabora mjini 

Akifungua kongamano hilo mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amesema Serikali itaendelea Kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo kimsingi vinadaiwa kuwaathiri wasichana kimwili na Kisaikolojia na hivyo kusababisha kuwadhorotesha kifikila na kiuchumi ikiwemo kuwania uongozi

"Jitihada za shirika la msichana initiative pamoja na serikali hazotaishia hapa kwa Sababu tunataka mtoto wa kike asome hadi elimu ya juu ili aepukane mimba za utotoni na ndoa za utotoni ili baadae akawe kiongozi bora wa kesho"Amesema Mwanri 

Aisha Uledi ni miongoni mwa wasichana walio hudhuria kwenye kongamano hilo amesema semina hiyo imewasaidia kwa kiasi kikubwa kwa wasichana na kujitambua na kuweza  kuwania nafasi za uongozi

Kwa Upande wake  Mkurugenzi mtendaji wa shirika la initiative msichana Rebeca Gyumi amesema kongamano hilo litaweza kusaidia jamii kuona ni jinsi gani msichana ataweza kuonesha na Kutumia nguvu zake mwenyewe kama chachu ya maendeleo kukomesha ukatili wa kijinsia 

Aidha mkoa wa Tabora ni miongoni mwa mikoa mitatu nchini inayoongoza kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ambapo shirika lisilo la kiserikali la Msichana Initiative linatekeleza Mpango wa kuwajengea uwezo wasichana  ili iwe kichocheo cha Kushiriki vita dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia hususani Mimba za utotoni pamoja na ndoa za utotoni.
 Pichani ni wasichana walioshiriki katika kongamano hilo la ajenda ya msichana mkoani Tabora.
Pichani ni mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akizungumza na wasichana (Pichani hawapo)  katika kongamano la msichana lililoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Initiative.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...