KCB Bank Tanzania imeendesha Kongamano la Biashara Club kwa mara ya pili jijini Mwanza ikiwa ni ni sehemu ya mikakati yao ya kutoa elimu ya usimamizi wa fedha, uendeshaji wa biashara na sheria za kodi kwa wafanyabiashara wadogo na wakati zaidi ya 200 wamepatiwa mafunzo hayo pamoja na kuwakutanisha na wafanyabisha wa ndani na nje ya nchi.
Kwa mujibu wa benki hiyo ni kwamba tangu kuzinduliwa kwake mwaka 2017, KCB Biashara Club imeendelea kuonesha dhamira yake ya kukuza biashara katika seckta ya SME kwa kutoa huduma bora za kibenki kwa wafanyabiashara wadogo na wakati yaani (SME) pamoja na kuwaonesha mbinu za kukuza mitaji ya shughuli zao za kibiashara. Semina hiyo iliyofanyika katika Hotel ya Gold Crest jijini Mwanza ilikusanya wafanyabiashara na wajasiriamali kutoka nyanja mbali na kwa pamoja walipata kufahamu fursa zinazotolewa na benki hiyo kwa wanachama wa Biashara Club.
 Akizungumza katika warsha hiyo iliyofanyika jijini Mwanza, Mkuu wa Idara ya Masoko, Mahusiano na Mawasiliano Christine Manyeye amesema: ”Dhumuni kubwa la Biashara Club ni Pamoja na kuwajengea wachama wake mahusiano bora ya kibiashara na wajasiriamali wenzao.”
Kwa upande wake Meneja wa Tawi, KCB Bank Mwanza, Emmanuel Mzava amewashukuru wafanyabiashara na wajisiriamali kwa kujitokeza kwa wingi kuja kupata mbinu muhimu zitakazowasaidia katika kukabiliana na changamoto za kibiashara. “Mtegemee semina kama hizi kwa siku za mbeleni kwani Mwanza ni jiji linaloonyesha kushamiri kibiashara” aliongezea Nd. Mzava.
Wakati  Saada Sipemba kutoka Sadio Travel and Tourism ambaye ni mtaalamu wa safari za kibiashara amesema fursa za kibiashara walizozipata wafanyabiashara 10 ambao walisafiri kwenda nchini China hivi karubuni. Amebainisha kuwa bila juhudi za benki ya KCB kuhakikisha inawatengenezea wateja wake mianya ya kutumia fursa hizo kwa urahisi, safari ya China isingekuwa ya mafanikio.
Benki ya KCB Tanzania kupitia Biashara Club imekuwa ikiandalia wadau wake safari za kibiashara kwenda nchi kama China, Malaysia na Afrika Kusini kwa gharama nafuu kwa dhumuni la kuwafungulia masoko mapya na bidhaa nafuu za kuleta kwenye soko la Tanzania.
 Mmoja wa Wateja na Mwanachama wa KCB Biashara Club Jonex Kinyonyi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Texas Hardware Limited alikiri kwamba Benki ya KCB imefanya kazi kubwa sanakatika kumsaidi kukuza biashara yake hadi kufikia kufungua kamouni ya pili inayojihusisha na maswala ya bima.
Kuhusu Benki ya KCB Benki ya KCB ni benki kubwa zaidi Afrika Mashariki na Kati iliyoanzishwa mwaka 1896 kisiwani Zanzibar. Toka hapo benki hiyo imekua na kuenea katika nchi za Tanzania, Kenya Sudani ya Kusini, Uganda, Rwanda, Burundi na Ethiopia.
Kwa sasa benki hiyo ina mtandao mkubwa zaidi katika kanda hii ikiwa na matawi 262, mashine za kutolea fedha (ATM) 962, na wakala 15,000 wanaotoa huduma za benki masaa 24 siku saba za wiki Afrika Mashariki. Benki ya KCB imesajiliwa katika soko la hisa la Nairobi, Dar es Salaam, Uganda na Rwanda. KCB Bank Group pia linamiliki kampuni ya bima ya KCB, KCB Capital na KCB Foundation. Nchini Tanzania, KCB ilifungua milango yake mwaka 1997 na toka hapo imekuwa mdau mkubwa katika kukuza sekta ya fedha nchini.

Kwa sasa benki ina matawi 14 Tanzania bara na visiwani Zanzibar. Matawi hayo ni Samora, Mlimani, Uhuru, Msimbazi, Lumumba, Buguruni, Oysterbay, Mbagala jijini Dar es Salaam; Moshi, Zanzibar, Arusha Main na TFA, Mwanza na Morogoro. Benki ya KCB Tanzania ni mlipa kodi mzuri, mwajiri wa watanzania zaidi ya 300,inafundisha wafanyakazi wake weledi wa kikazi na pia pale inapotokea nafasi inapeleka wafanyakazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...