Na Said Mwishehe,Michuzi Globu ya jamii

BAADA ya wananchi wa Msamvu mkoani Morogoro kutoa malalamiko kuhusu mchakato wa utolewaji wa vitambulisho vya Taifa, Rais Dk.John Magufuli amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Dk.Arnord Kihaule kufika leo leo Novemba 20,2019 mkoani hapo kutafuta ufumbuzi haraka ili wananchi wapate vitambulisho.

Mbali ya kwenda mkoani Morogoro Mkurugenzi huyo wa NIDA,Rais Magufuli amemtaka ndani ya siku tatu kuandaa utaratibu mzuri ambao utatumika nchi nzima katika kuharakisha upatikanaji wa vitambulisho hivyo ili wananchi wasajili laini zao za simu.

Akiwa eneo la Msamvu leo Novemba 20,2019, akiwa njiani kuelekea mkoani Dodoma, Rais Magufuli alipata malalamiko ya wananchi kutopata vitambulisha vya NIDA na kumekuwa na idadi kubwa ya wananchi ambao wanatoka maeneo mbalimbali ya Mkoa huo.

Hivyo ,Rais Magufuli aliamua kumpigia simu Mkurugenzi huyo na kumuelezea changamoto na baada ya kumaliza kuzungmza naye akatoa maagizo ambayo ametayaka yafanyiwe kazi haraka.

"Nataka Mkurugenzi Mkuu wa NIDA ufike hapa Morogoro ili ushughulikie hii changamoto ya vitambulisho , nimeelezwa ofisi ya NIDA mkoa wote wa Morogoro iko moja tu, hivyo watu wanatoka mbali kuja mkoani kufuata vitambulisho.

"Haiwezekani watu wasafiri kutoka wilayani kuja mkoani.Ofisi za NIDA ziwe kila mahali huko wilayani.Kama vipi muwape nauli na hela ya gesti.Ufumbuzi wa changamoto hii ufanyike hapa Morogoro lakini na wilaya zote nchini,"amesema Rais Magufuli.

Amesisitiza watu wanataka kusajili laini zao na mambo mengine, hivyo haiwezekani waliopewa jukumu hilo watashughulikie ili wananchi wapate vitambulisho na kisha waendelee na majukumu yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...