Afisa wa mahusino wa kampuni ya Infinix, Aisha Karupa  Akizungumza na vyombo vya habari wakati wa uzinduzi wa Infinix S5, jijini Dar es Salaam. Alisema kuwa msimu huu wa sikukuu za Christmas na Mwaka mpya hivyo Infinix kusheherekea pamoja.
 Afisa wa mahusino wa kampuni ya Infinix, Aisha Karupa  akionesha simu iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam.




Baadhi ya wateja wakiangalia ubora wa simu iliyozinduliwa.

 INFINIX, baada ya kuliteka soko na toleo pendwa la Infinix S4, Infinix imezindua rasmi Infinix S5, kinamara wa toleo la S series kwa sasa ikiwa na Infinity-O Display na 32MP.

 Ujio wa Infinix S5 umeambatana msimu wa sikukuu za Christmas na Mwaka mpya hivyo Infinix kusheherekea msimu huu kwa kuzindua rasmi promotion itayoanza rasmi tarehe 25/11/2019 na zawadi mbalimbali kama vile Vacuum Cleaner, Deep Flyer, Subwoofer Radio.

Akizungumza na vyombo vya habari wakati wa uzinduzi wa Infinix S5, Afisa wa mahusino wa kampuni ya Infinix, Aisha Karupa alisema, “Infinix ikiwa ni kampuni yenye ushawishi mkubwa katika mfumo wa kidigitali tunawahakikishia wateja wetu bidhaa zenye teknolojia ya hali ya juu kwa bei Rafiki”,Vile vile Aisha aligusia kuhusiana na sifa za simu hiyo kwa kusema, “na pamoja ya kuwa na selfie kali yenye 32MP lakini pia inasifa lukuki kama vile teknolojia ya Artifficial Intelligence kwenye kamera 4 za

nyuma ambazo ni 16MP+5MP+2MP+AI Lens, lakini pia Infinix S5 ina memory card ya ukubwa wa GB 4 kwa GB64 yenye uwezo wa kutunza kumbukumbu nyingi pasipo huitaji ya memory card ya ziada na kwa upande wa design Infinix S5 imekuja katika muonekano wa kitofauti wenye kuvutia kutokana na namna kamera ya mbele ilivyopachikwa ndani ya Display kwa jina la kitaalamu Infinity-O Display na kwa wale wenye matumizi mengi Infinix S4 inauwezo wa kukaa na chaji kwa muda mrefu kutokana na ujazo mkubwa wa Battery wenye mAh40,000”.

Pia Infinix wametumia nafasi hiyo kutambulisha rasmi promotion ya msimu wa sikukuu inayoenda sambamba na uzinduzi wa Infinix S5. Akizungumza meneja wa mauzo wa Infinix Bwana Fredy Kadilana alisema kwamba, katika msimu huu wa sikukuu za Christmas na mwaka mpya Infinix imezindua rasmi promotion itakayompa nafasi mteja wa Infinix S5 au mteja wa simu yoyote ya Infinix kujishindia zawadi mbalimbali kama vile Vacuum Cleaner, Deep Flyer, Subwoofer Radio na nyengine nyingi lakini pia Infinix haijasahau wadau wake wa wanaotembelea kurasa @infinixmobiletz kwa kuitambulisha challenge ya #S5showitoff itayoanza rasmi mwishoni mwa wiki hii”.

Kwa maelezo zaidi tembelea www.infinixmobility.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...