MLIMBWENDE wa Utalii lazima awe na sifa, vigezo na masharti ambazo zinakidhi vigezo vya kimataifa kwaajili ya kuwakilisha nchi katika utalii wetu hapa nchini.
Ameyasema hayo Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu
wakati wa ufunguzi wa semina ya kuwajengea uwezo wahariri na waandishi wa habari kwaajili ya kuandika habari zinazokidhi vigezo vya ulimbwende wa utalii. Semina hiyo imefanyika katika hoteli ya kitalii ya Jaromax iliyopo Mazese jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wa wazazi na walezi wa walimbwende watakao ingia katika kinyang'anyilo hicho Kanyasu amesema kuwa hawfikilii tena kuwa mziki ni uhuni, na walimbwende wenyewe waidhiilishie jamii kuwa shughuli za urembo sio kujidhalilisha.
Hata hivyo Afisa sanaa wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Bona Masenge, amesema kuwa mchakato wa usaili wa kumtafuta mlimbwende wa urembo katika utalii (Miss Tourism) kuanza Desemba, 2019.
Bona amesema kuwa BASATA imewaamini waandaaji wa Shindano la Miss utalii kwani kunavigezo mbalimbali ambavyo wamekidhi vya kikanuni, kisheria na kwaajili ya kuandaa shindano hilo.
"Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) linahusika na mashindano haya kwa ukaribu ili kuhakikisha waandaaji wa mashindano haya wanakidhi vigezo na kufata taratibu na sheria zilizowekwa na Baraza".
Amesema Bona
Bona amesema kuwa Shindano la Mlimbwende wa Utalii limeweza kuwapa ajira za kudumu vijana kwa kuinua vipaji vya vijana wengi na kukuza utalii hapa nchini.
"Mashindano ya mlimbwende wa Utalii yameweza kuinua vipaji kwa washiriki na baadhi wameweza kupata ajira za kudumu na yameweza kukuza utalii kitaifa na kimataifa".
Kwa upande wake Rais wa shindano la miss Utalii, Gideon Chipungahelo amesema kuwa Shindano la Mlimbwende wa utalii tukitaka mabadiliko katika urembo ni lazima kufanya mambo mazuri zaidi ya urembo na kuwawezesha washiriki kuwa na maarifa mengi ya masuala ya Utalii.
Amesema watakaohitaji kushiriki Mahindano hayo wakae mkao wa kula kwani tunata yanayotakiwa ni Mapinduzi Makuwa katika tasnia nchini.
"Miss yourism Tanzania (Mlimbwende wa utalii Tanzania) historia yake kabla na baada ya uhuru shindano la kwanza la kupata mshindi wa dunia katika ulimbwende wa Utalii.
Amesema Chipunagahelo.
Hata hivyo mchakato huo wa kutafuta Mlimbwende katika utalii utachukua zaidi ya Miezi sita ili kuwapa muda majaji kufanya kazi ya kutafuta Mrembo anayekidhi vigezo vyote na atakayetuwakilisha duniani na kutuletea taji la dunia hapa nchini.
Baadhi ya Walimbwende wa 2013 na 2014 walioshiriki katika Shindano waliohudhulia semina ya waandano la Miss Utalii.
Rais wa shindano miss Utalii, Gideon Chipungahelo akizungumza wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wahariri na waandishi wa habari, katika hoteli ya kitalii ya Jaromax iliyopo Manzese jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa Shindano la Mlimbwende wa utalii tukitaka mabadiliko katika urembo ni lazima kufanya mambo mazuri zaidi ya urembo na kuwawezesha washiriki kuwa na maarifa mengi ya masuala ya Utalii.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Costantine Kanyasu akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa Shindano la kutafuta mlimwende katika utalii (Miss Tourism), katika Hoteli ya Kitalii ya Jaromax iliyopo Manzese jijini Dar es Salaam.
Afisa sanaa wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Bona Masenge akizungumza wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wahariri na waandishi wa vyomo vya haari jijini Dar es Salaam katika hoteli ya kitalii ya Jaromax iliyopo Mazese jijini Dar es Salaam.
Rais wa Sanaa za Maonesho, Wilium Chitanda akizungumza wakati wa Semina ya kuwajengea uwezo wahariri na waandishi wa vyombo vya habari hapa nchini kwaajili ya kuandika habari za Miss Utalii kwa uelewa zaidi. Semina hiyo imefanyika katika Hoteli ya Kitalii ya Jaromax iliyopo Manzese jijini Dar es Salaam.
Rais wa shirikisho la Sanaa za Ufundi Tanzania(TAFCA), Adrian Nyangamawe akizungumza katika semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari katika habari za mlimbwende wa Utalii (Miss Tourism) katika semina iliyofanyika hoteli ya Kitalii ya Jaromax iliyopo Mazese jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Walimbwende wa 2013 na 2014 walioshiriki katika Shindano waliohudhulia semina ya waandano la Miss Utalii.
Moja ya watoa Mada katika Semina ya kuwajengea uwezo wahariri na waandishi wa habari.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...