Na Khadija Seif, Michuzi TV

MWAMUZIKI  nguli wa Bongofleva Hamis Mwinjuma  a.k.a Mwana FA amesema wasanii waache lawama kipindi kazi zao zinapofungiwa katika baraza la Sanaa (BASATA).

Mwana FA  (pichani) ameyasema hayo katika mahoijiano maalumu, kufuatia minong'ono inayoendelea ya yeye kuhusishwa na ufungiwaji wa kazi za wasanii Basata.

"Mimi ni mjumbe tu wa baraza la Sanaa (BASATA) sihusiki na jukumu la kumfungia mtu kazi zake na wala sina ofisi pale basata kwahiyo wasanii wasinitupie lawama najaribu kufanya kazi na utaratibu ambao baraza kama baraza huwa wananipangia na mara nyingi nimekua  kama mshauri kwa wasanii wenzangu linapotokea tatizo lolote lile", amesema.

Mwana FA  ametaja changamoto kadhaa ambazo wanazipata wasanii wachanga ni ikiwa ni pamoja na tuzo zinazotolewa na kuwepo dhana na ukandamizwaji au kubaguliwa na amemtaja Marehemu Sam wa Ukweli kama kielelezo tosha.

"Kuna tuzo zilikuwepo na katika kinyang'anyiro hicho Marehemu Sam wa Ukweli alikua akishiriki na ikaonekana wazi wazi kuwa wamembania na kumnyima tuzo wakati ni kitu ambacho Mashabiki wanajua alistahili hivyo kwa namna moja au nyingine ilimvunja moyo na kumrudisha nyuma kimuziki," ameelez.

Mwana  FA alichukua nafasi hiyo kuwapongeza  Watanzania wote kwa uzalendo walioonyesha na kuhamasika kujaa uwanjani na kumshangilia bondia Hassan Mwakinyo usiku wa kuamkia  novemba 30 Mwaka huu.

"Wakati mwengine tukiwa pamoja na tukijenga nguvu katika michezo yetu na kuwapa moyo wachezaji huwa wanajitoa na kuona nia ya kuwakilisha Taifa na kulitoa kimasomaso kutokana na hamasa wanazozipata", ameeleza Mwana FA ambaye pamoja na msanii Ommy Dimpoz, Ney wa Mitego na Profesa Jay walikuwa mstari wa mbele  katika kutoa hamasa kwenye mpambano huo ambao Mwakinyo alishinda kwa pointi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...