Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa pili kulia) akikata utepe kuashiria kuwashwa kwa umeme katika mtaa wa Konje shule.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati) akiongea na wananchi wa kijiji cha Kwedikabu baada kumaliza kukagua mgodi wa Kusini Gateaway. kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe.

Wananchi wa Kata ya Konje wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani) kwenye hafla ya kuwasha umeme katika Kata hiyo

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akishuka ngazi mara baada ya kukagua moja ya majengo ya mgodi wa Kusini Gateaway.

**********************************

Na Hafsa Omar – Tanga

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, Novemba 20 mwaka huu, ameendelea na ukaguzi wa kazi ya usambazaji umeme vijijini ili kuhakikisha kuwa lengo la Serikali kupeleka umeme katika vijiji vyote linafanikiwa.

Katika ziara hiyo, alikagua kazi husika katika Kata ya Konje, Kata ya Bwawani na mgodi wa dhahabu wa Kusini Gateway uliopo katika kijiji cha Kwedikabu, kitongoji cha Msenga, Wilaya ya Handeni, mkoani Tanga na kuwasha umeme katika mtaa wa Konje Shule na mtaa wa Kwamneke.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kwedikabu alisema, nia ya ziara yake kwenye mgodi ni kuhakikisha kwamba maeneo hayo ambayo yana faida nyingi kiuchumi nchini, yanapelekewa miundombinu ya umeme.

Aidha, alilitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuharakisha kupeleka umeme kwenye eneo hilo la mgodi, kwani shirika hilo litajiongezea mapato, ambayo yatasaidia kusambaza umeme kwenye maeneo mengine.

Aliongeza kuwa, wawekezaji wengi wa madini ambao bado huduma ya umeme haijawafikia katika maeneo yao, watashawishika kujiunga na huduma hiyo mara baada ya umeme kufika katika eneo hilo, na itakuwa faida kubwa kwa TANESCO, ambayo kwasasa inajiendesha yenyewe bila kutegemea ruzuku kutoka Serikalini.

“Mimi nataka niseme nimekuja kwenye eneo ambalo linaweza kuongeza mapato,na ukizingatia kuwa umeme ni huduma lakini pia ni biashara, kwa hiyo tupo kutafuta masoko na soko tumelikuta hapa.”

Naye Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe aliishukuru Serikali kwa kazi ya usambazaji wa umeme katika wilaya ya Handeni, ambapo alisema hapo awali walikuwa wanategemea umeme kutoka Hale na Korongwe lakini kwasasa, Serikali imewapelekea vituo viwili vya kupozea umeme.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...