Wakati
kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa zikiendelea nchini, aliyekuwa Meya wa
Jiji la Arusha Kalisti Lazaro amejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na
kupokelewa na Ndg. Humphrey Polepole Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM.
Ndugu
Kalisti Lazaro aliyefika katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba
jijini Dar es Salaam ameeleza amefikia uamuzi huo baada ya kupitia wakati mgumu
akiwa katika Wadhifa wake wa Meya wa Jiji la Arusha.
Ndugu
Kalisti amesema amepokea barua za maonyo mara kadhaa kutoka Uongozi wa Chama
Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambazo zilimtaka kutokutoa ushirikiano na
Viongozi wa Serikali ambao anatakiwa kufanya nao kazi ngazi ya Mkoa na Wilaya
na kutompongeza hadharani Ndg. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa kazi nzuri ambayo ameifanya Nchini ikiwamo katika Mkoa
wa Arusha.
Vitisho
vya mara kwa mara ikiwamo dhidi ya uhai wake ndio vimepelekea kujivua nafasi
zake zote katika Chadema na kujiunga na CCM, Chama ambacho kinashughulika na
utatuzi wa kero za wananchi. Ndg. Lazaro pia amechukizwa na Chama chake kujitoa
katika uchaguzi huku akiita kitendo hicho uvunjaji wa demokrasia ambacho ndani
ya masaa mawili uamuzi wa Kamati Kuu ya Chadema iliwanyima mamilioni ya wapenda
demokrasia haki ya kushiriki katika Uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa, Vijiji
na Vitongoji.
Ndg.
Kalisti Lazaro amesema sasa yuko tayari kuchapa kazi ya wananchi akiwa ndani ya
Chama ya Mapinduzi na kwamba yuko tayari kwa maelekezo ya kazi kutoka Uongozi
wa CCM.
Ndg.
Kalisti kwa kujiunga na CCM amejiuzuru nafasi ya Udiwani, Umeya wa Jiji la
Arusha, Uenyekiti wa Mameya na Madiwani wote wa Chadema Nchini na Ujumbe wa Kamati Kuu ya
Chadema.
Ndugu
Kalisti Lazaro atapokelewa rasmi na wanachama wa CCM Mkoa wa Arusha katika
tarehe itakayopangwa hivi karibuni.
Imetolewa
na,
IDARA
YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA
CHA MAPINDUZI (CCM)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...