Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa (kulia) akimpongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kumtunuku Shahada ya Heshima ya Uzamivu (PhD) katika Sayansi, wakati wa Mahafali ya 10 ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) leo tarehe 21/11/2019 jijini Dodoma. Katikati ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Prof.Josephat Bee.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Cheti cha Shahada ya Udaktari wa Falsafa (PhD) kutoka kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa mara baada ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu (PhD) katika Sayansia wakati wa Mahafali ya 10 ya chuo hicho leo tarehe 21/11/2019 jijini Dodoma. Rais Magufuli ametunukiwa PhD hiyo ikiwa ni kutambua mchango wake katika maendeleo ya nchi ambapo anakuwa mtu wa tatu kutunukiwa Shahada hiyo na UDOM akitanguliwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Mrisho Kikwete na Mzee Rashid Mfaume Kawawa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...