Na, Editha Edward -Tabora

Serikali kupitia wizara ya maliasili na utalii imesema inaendelea na mikakati ili Kuhakikisha kunakuwa na Masoko ya Uhakika ya Asali kwa kuanzisha viwanda katika maeneo mbalimbali Nchini ambapo tayari imetenga bajeti ili Kuanza ujenzi wa viwanda viwili na kukarabati viwanda vingine vitano vilivyopo

Akizindua kamati ya kitaifa ya ushauri wa masuala ya ufugaji nyuki mjini Tabora yenye wajumbe wapatao kumi waziri Kigwangala amebainisha kuwa kuna haja ya kuwa na viwanda vya kuchakata na kufungasha Asali vitakavyosaidia kuwa na Masoko huku akisisitiza umuhimu wa kuwa na mfumo thabiti wa vyama vya ushirika ili visimamie viwanda hivyo ambapo ametoa muda wa mwezi mmoja Kuhakikisha kuna mifumo ya ushirika

"Pesa zimetengwa taasisi zipo na zipo tayari kuchangia mizinga zipo tayari kwa ajili ya kujenga hivyo viwanda lakini mfumo haupo mimi nilichokitaka nikuwepo na mfumo thabiti wa ushirika kwani ndiyo msingi wa kufanikiwa kwenye utekelezaji wa mpango huh"Amesema Kigwangala 

Katika hatua nyingine Waziri Kigwangala amekabidhi Mizinga miasita kwa kikundi chat ufugaji nyuki IPOLE na mizinga miatano katika chuo cha ufugaji nyuki Tabora huku akiziagiza taasisi zilizo chini ya wizara yake zikuwemo TANAPA, TAWA na TFS kutengeneza mizinga elfusita Kila taasisi ili zigawiwe katika vyama vya ushirika vitakavyoanzishwa 

Kwa upande wake Katibu mkuu wizara ya maliasili na utalii Ezekiel Mwakalukwa Amesema takwimu zilizopo za mizinga katika kikundi chat Ipole ni takribani elfu kumi na mbili ya magome ya miti na mizinga ya maboxisi ni mizinga miamoja licha ya kuwepo na juhudi kubwa ya ufugaji nyuki lakini kwa sehemu kubwa inaharibu Mazingira

Aidha pamoja na kukabidhi mizinga Huyo waziri wa maliasili na utalii pia ameiomba bodi kumshauri kuhusu ujenzi wa viwanda na muundo mzuri ambao utafaa katika kuvisimamia na namna ya upatikanaji wa Masoko ya Uhakika. 
Mizinga ya nyuki miatano iliyokabidhiwa kwenye chuo cha ufugaji nyuki Tabora
Waziri wa maliasili na utalii Dkt Hamis Kigwangala akikabidhi mizinga miasita kwa kikundi cha ufugaji nyuki IPOLE
Waziri wa maliasili na utalii Dkt. Hamis Kigwangala akizungumza katika uzinduzi wa kamati ya kitaifa ya ushauri wa masuala ya ufugaji nyuki mjini Tabora
wajumbe wa kamati ya ushauri wa masuala ya ufugaji nyuki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...