Na Karama Kenyunko, globu ya jamii.
BAADA ya zao la Tumbaku kulimwa na kupitiliza malengo ambayo yalipelekea baadhi kushindwa kupata mnunuzi  hatimae serikali kwa juhudi zake imefanikiwa  kupata makampuni mawili kutoka nchi jirani ya Zambia kuja kununua zao hilo la Tumbaku iliyobakia kutoka kwa wakulima

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga amesema zao la Tumbaku ni moja ya mazao ya kimkakati ambayo yanalimwa kwa mkataba ambapo makampuni yanajitojeza kununua mapema na kusaini mkataba.

Amesema msimu uliopita uzalishaji wa Tumbaku  ulipitiliza malengo yaliyowekwa ambapo zaidi ya tani elfu tatu zilibaki baada ya makampuni kuchukua ile waliyokuwa wameingia mkataba hivyo serikali ikalazimika kufanya juhudi za kutafuta wanunuzi.

“Katika msimu uliopita lengo la uzalishaji katika mkataba lilikuwa ni tani 57,305.1, wakulima walizalisha kilo 12,452.3 zaidi ya malengo ya mkataba lakini kutokana na mkataba kampuni  inatakiwa kununua asilimia kumi zaidi ya malengo tuliyokubaliana na mpaka kufikia mwishoni mwa msimu makampuni yalikuwa yamenunua  tani 60, 691.9. sawa na asilimia 105 ya makubaliano.

Amesema, serikali ilitafuta wanunuzi wa tumbaku iliyobaki ambapo  kampuni ya Alliance One na Premium Active ziliongeza jumla ya tani 6,305 na kufanya kiasi cha Tumbaku iliyobaki kufikia tani 3,345.1.

Ameeleza kuwa, kuwa juhudi za serikali hazikuishia hapo kwani walifanikiwa kushawishi kampuni za Topper Leaf Company na Tombwe processing kutoka Zambia kuja kununua tumbaku iliyobaki ambapo sasa hivi wako katika hatua za kusaini mkataba kwa ajili ya kununua tumbaku hiyo.

Aidha ameongeza kuwa, serikali imejipanga vema katika msimu ujao ambao masoko yake yataanza Mei mwakani na  kampuni za ununuzi zilizopo Tanzani ambazo ni Alliance One, Premium Active na Japana Tobacco International zimetoa mikataba ya tani  42,225.9 kiasi ambacho ni kidogo kutokana na kujitoa kwa kampuni ya Tanzania Leaf Tobacco Company (TLTC) katika ununuzi wa Tumbaku.

 Hasunga aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo serikali ilifanya juhudi za kutafuta kampuni zaidi na kufanikiwa kushawishi kampuni nyingine nne  kutoka Zambia zitakazowezesha kufikia matarajio ya tani 63278.6 msimu ujao.
“Tumefanikiwa kuongeza kampuni nne kutoka Zambia kupitia kampuni za kizawa na hivyo tunatarajia malengo ya mikataba ya msimu ujao yatatimia,” alisema.
Akiekeza  sababu za kujitoa kwa kampuni ya TLTC alisema ni kupungua kwa mtaji kulikotokana na deni la faini walilotozwa na Tume ya ushindani pamoja na fedha za VAT ambazo hawajarejeshewa kutokana kutofautiana kwa mahesabu na serikali.

Aidha amesema kuwa sasa hivi serikali imesema iko mbioni kununua ndege ya mizigo itakayowezesha kusafirishwa kwa mazao ya mboga mboga mboga na matunda kwenda nje ya nchi ili yaweze kufika yakiwa katika hali nzuri na kuongeza uchumi wa nchi.
 Waziri wa Kilimo Josephat Hasunga akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 30, 2019 jijini Dar es  Salaam alipokuwa akitoa taarifa juu ya kupatikana kwa makampuni mawili ya kutoka nchini Zambia yaliyojitokeza kununua Tumbaku iliyobaki msimu uliopita baada ya kupitiliza malengo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...