Serikali imeridhia kupeleka vikosi maalumu vya ulinzi maeneo ya mipaka ya vijiji Wilayani Tandahimba
Akizungumza na wananchi wa kata ya Michenjele na Mihambwe Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba alisema kuwa vikosi hivyo vitakuja wakati wowote
"Nimekuja kuzungumza nanyi kuwa serikali imeridhia ombi la kuleta Majeshi ya Ulinzi katika maeneo ya huku mipakani kwa kutambua kuwa Wilaya yetu imepakana na nchi ya Msumbiji na kwa Sasa Msumbiji hakuna amani "alisema Waryuba
Alisema kuwa tayari Jeshi la Polisi limeweka kambi katika kata ya Namikupa ambapo wameona ni katikati katika shughuli zao za ulinzi.
Waryuba alisema ujio wao utakuwa ni kuangalia sehemu sahihi ya kuweka kambi ya kikosi maalum wakishajiridhisha ndipo watakuja rasmi
"Toeni ushirikiano ili vikosi vije tuishi kwa amani,usalama na utulivu katika maeneo yetu maana Hadi Sasa bado watu wanashindwa kwenda mashambani kwa hofu,"alisema Waryuba
Naye mkazi wa ng'ongo Dadi Tipila ameishukuru serikali kwa niaba ya wanamichenjele kwa hatua iliyochukuliwa na serikali kuhusu vijiji hivyo
" Tangu tukio la wenzetu kuuwawa bado tunayo hofu tunashindwa kwenda shambani kwa amani,tunaahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa vikosi vya ulinzi pale watakapo hitaji msaada kutoka kwetu,"alisema Tipila
Hatua ya kuimarisha ulinzi katika vijiji vya mipakani ndani ya Wilaya ya Tandahimba imekuja baada ya watu sita kuuawa na watu wasiojulikana .
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba akizungumza na wananchi wa kata ya Mihambwe
Wananchi wa Mihambwe wakimsikiliza DC wa Tandahimba
Wananchi wa Michenjele wakimsikiliza Dc






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...