Ndajiri Lonyori kutoka shule ya
secondari Orkeeswa akipokea kombe la ushindi wa mchezo wa mpira wa
kikapu wa wasichana chini ya miaka 19 wakati wa wikiendi ya michezo kwa
shule za kimataifa iliyofanyika mkoani Moshi wikiendi hii. Shule ya
sekondary Orkeeswa kutoka mkoani Arusha iliibuka kidedea baada ya
kuchota makombe 15 katika michezo mbalimbali iliyoshiriki.
Ndajiri Lonyori kutoka shule ya
secondari Orkeeswa akionyesha kombe lao la ushindi wa mchezo wa netball
chini ya miaka 15 wakati wa wikiendi ya michezo kwa shule za kimataifa
iliyofanyika mkoani Moshi wikiendi hii. Shule ya sekondary Orkeeswa
kutoka Arusha iliibuka kidedea baada ya kuchota makombe 15 katika
michezo mbalimbali iliyoshiriki.
Amani Isaya kutoka shule ya sekondary
Orkeeswa akionyesha kombe lao la ushindi wa mchezo wa volleyball chini
ya miaka 19 wakati wa wikiendi ya michezo kwa shule za kimataifa
iliyofanyika mkoani Moshi wikiendi hii. Shule ya sekondary Orkeeswa
kutoka Arusha iliibuka kidedea baada ya kuchota makombe 15 katika
michezo mbalimbali iliyoshiriki.
Emmanuel Meibuko golikipa wa timu ya shule ya
sekondari Orkeeswa akipokea kombe la ushindi wa mpira wa miguu wa
wavulana chini ya miaka 19 baada ya kuibuka washindi kwa goli 3 - 2
katika mechi iliyokuwa ngumu sana kwa vijana hao wakati wa wikiendi ya
michezo kwa shule za kimataifa iliyofanyika mkoani Moshi wikiendi
hii. Shule ya sekondary Orkeeswa kutoka Arusha iliibuka kidedea baada ya
kuchota makombe 15 katika michezo mbalimbali iliyoshiriki.
Shule
ya Secondari Orkeeswa iliyopo mkoani Arusha iliibuka kidedea baada ya
kuchota makombe 15 katika michezo mbalimbali ya Shule za Kimataifa.
Shule
hizo kutoka mikoa mbalimbali nchini zilikutana mkoani Kilimanjaro na
kuchuana vikali katika michezo ikiwemo mpira wa kikapu, mpira wa miguu, tennis,
swimmings, netball, volleyball, frisbie, rugby na michezo mingineyo.
Timu za kikapu U19
wasichana na U19 wavulana pamoja na timu ya mpira wa miguu ya shule hiyo
zilionekana kuwa imara zaidi baada ya kushinda kwa kishindo timu za
shule mbalimbali zilizo pambana nao.
Shule za kimataifa nchini zilikuwa na
wikiendi ya michezo iliyoanza mwishoni mwa wiki,Ijumaa na kufikia tamati Jumapili.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...