Madarasa yaliyoezuliwa na mvua shule ya msingi Namindondi.
Shule ya Namindondi iliyopo Wilaya ya Tandahimba imeezuliwa paa na mvua wakati wanafunzi wa darasa la nne wakifanya Mtihani wa Taifa
Akizungumza na kutoa maelekezo katika eneo la tukio,
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tandahimba Said Msomoka amesema kuwa tayari hatua za utekelezaji zimechukuliwa ili kuhakikisha Wanafunzi wanaendelea na masomo
"Tunashukuru hakuna mwanafunzi aliyeumia na wanafunzi waliendelea na mitihani kwa kuhamishiwa darasa lingine,kwa hiyo utekelezaji utaanza rasmi kesho ili hadi kufikia jumatatu wanafunzi waendelee na masomo,"alisema Msomoka
Naye Kaimu Mkuu wa shule Juma Kasidi alisema mvua hiyo ilikuwa yenye upepo mkali iliyoambatana na radi ilisababisha uharibifu wa madarasa matatu likiwemo darasa la nne ambalo walifanyia Mtihani wa Taifa
"Ilikuwa muda wa mchana wakati darasa la nne wanamalizia Mtihani wa Taifa, somo la maarifa ya jamii ndipo tukio hilo lilitokea na hivyo tuliwahamishia wanafunzi darasa lingine wakaendelea na mitihani,hakuna aliyejeruhiwa,"alisema Kasidi
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tandahimba Said Msomoka akitoa maelekezo kwa Mwenyekiti wa bodi ya shule
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tandahimba Said Msomoka akitoa maelekezo kwa Mwenyekiti wa bodi ya shule
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...