Klabu ya Soka ya Simba rasmi imeachana na Kocha wake Mkuu, Patrick Aussems baada yakuvunja mkataba wake kutokana nakushindwa kutekeleza majukumu yake kwa viwango na malengo ambayo Klabu hiyo ilikubaliana naye kwenye mkataba wa ajira.
Taarifa ya Klabu hiyo iliyotolewa leo kuhusu kuachwa kwa Kocha huyo imeeleza kuwa licha ya jitihada za Bodi ya Klabu hiyo kumpa ushirikiano Kocha huyo alisimamia timu hiyo bila kujali malengo ya Klabu, maamuzi hayo yamefanywa siku tano tangu kusimamishwa kwake kwa maswala yakinidhamu.
Taarifa hiyo imeeleza maelezo ya Kocha huyo yaliyotolewa mbele ya Kikao cha Kamati ya Nidhamu Novemba 28 mwaka huu hayakuiridhisha Kamati hiyo dhidi ya tuhuma za Kocha huyo kuondoka Kiktuo cha Kazi bila ruhusa ya Uongozi wa Klabu licha yakukataa kuiambia Kamati sehemu alipokuwa na sababu za kwenda bila ruhusa.
Simba SC kupitia taarifa hiyo imesema itaanza mara moja mchakato wakutafuta mbadala wa Kocha Mkuu, tayari Kocha Msaidizi, Dennis Kitambi ameteuliwa Kukaimu nafasi hiyo ya Kocha Mkuu hadi atakapopatikana mwengine.
Katika hatua nyingine, Klabu ya Mbeya City ya Mbeya imeridhia kujiuzulu kwa Kocha Mkuu, Juma Mwambusi baada yakuwasilisha ombi lake lakujiuzulu tangu Novemba 26 mwaka huu.
Kupitia taarifa ya Klabu hiyo iliyotolewa leo imeeleza kuwa Mwalimu Mwambusi aliwasilisha ombi hilo kufuatia mwenendo wa timu usioridhisha tangu kuanza kwa Ligi Kuu msimu huu.
Pia, Mbeya City imemkabidhi timu hiyo, Kocha Msaidizi, Mohammed Kijuso wakati mchakato wakutafuta Kocha mpya ukiendelea.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...