Joseph Kinduguyo ambaye ni muhasisi wa kampuni ya kampuni ya larittate Legal Consultants akiendelea kuwapa semina washiriki.
Washiriki wakifuatilia semina hiyo 


Na Woinde Shizza, globu ya jamii Arusha

Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega ameagiza taasisi zilizo waajiri watumishi kuhakikisha maeneo yao ya kazi wanapa stahiki zao kutokana na namna wanavyofanyakazi kwenye idara kwa lengo la kuondoa changamoto zinazowakabili za kulalamikia maslai madogo wanayolipwa,

Kwitega ametoa Agizo hilo wakati wa ufunguzi wa Semina ya kuwajengea waajiri uwezo wa kufuata taratibu za kazi ikiwemo misingi bora kwa watumishi mkoani Arusha na kusema kwamba malalamiko makubwa hutokana na mashirika ya watu binafsi kushindwa kuheshimu mikataba ya kazi na kupelekea kufungua majalada mahakamani.

Ameeleza kuwa mbali na jitihada ambazo zimekuwa zikifanywa na serikali kutatua malalamiko kwa watumishi wa sekta binafsi kwa kutoa ushauri wa kisheria lakini bado kumekuwepo na changamoto hivyo ameitaka kampuni ya Clarittate Legal Consultants inayo endesha semina hiyo kuwapa mafunzo taasisi zinazohudumia jamii kwani kampuni hiyo imekuwa ikisaidia taasisi kufuata taratibu kanuni na miongozo jinsi ya kufanyakazi kwa mujibu wa sheria za nchi

Katibu tawala amesema kuwa waajiri waliopata mafunzo hayo endapo watatumia vyema elimu walipata itasaidia kuondoa migogoro na migongano katika taasisi hivyo mafunzo hayo ni mwanzo mzuri wa kuondokana na migogoro ya mara kwa mara kati ya mwajiriwa na bosi wake.

Awali akizungumza semina hiyo kwa waajiri hao mwanasheria Emmanuel Atonny Ngeiza amesema kwamba waajiri wengi wamekuwa wakifanya maamuzi kwa watumishi wao bila kuangalia maslahi ya mtumishi wake ni yapi na baadae wakijikuta wakitengeneza migogoro isiyo na tija kwa mtumishi kumfikisha mwajiri wake mahakamani kutafuta haki ya kulipwa stahiki zake.

Ngeiza amesema semina hiyo kwa waajiri imelenga kufuata taratibu za kazi pamoja na kuheshimu kazi zinazofanywa na mtumishi wake na endapo mtumishi ameachishwa kazi anapaswa kupata stahiki zake kwa mujibu wa sheria.

Naye mwazilishi wa kampuni hiyo Joseph Kinduguyo ambaye ni mwanasheria wa kujitegema amesema kumekuwepo na ukiukwaji wa kutokufuata sheria kanuni na miongozo ya kazi kwa waajiri walio wengi na hii ni mara baada ya kufanya utafiti wakaona umuhimu wa kutoa mafunzo kwa waajiri katika mikoa ya Arusha Kilimanjaro ili kuwapa mafunzo ya kuondoa changamoto zinazowakabili waajiri dhidi ya watumishi engo nikufikia mikoa yote nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...