Anaandika Abdullatif Yunus wa Michuzi TV.

Miongoni mwa masuala ya Kijamii yanayopewa kipaumbele kwa sasa ni pamoja na suala la Afya, ambapo kwa kutambua hilo Umoja wa Maendeleo ya Wanawake wa Kiislamu Kagera (UMWAKIKA) Kupitia Sadaka zao na waumini wengine pamoja na madhehebu mengine, wanaendelea na Ujenzi wa Hospitali ya Mama na Mtoto inayojengwa katika Kata ya Nyanga, Manispaa ya Bukoba.

Hajat Faidha Kainamula ni Mwenyekiti wa UWT - CCM Mkoa Kagera, akiwa Mgeni Rasmi katika Jaula na Harambee ya Uchangiaji wa Ujenzi iliyofanyika Hamugembe Manispaa ya Bukoba, amefurahishwa na jitihada za akina na mama Hawa zenye lengo la kumkomboa Mwanamke juu ya huduma anayopatiwa, akiongeza kuwa Hospitali zimekuwa zikiwadhalilisha akina mama katika utoaji wa huduma, bila kujali Dini zao, lakini kukamilika kwa Hospitali ya Nyanga utakuwa mkombozi juu ya stara ya akina Mama wote.

Katika Tamasha hilo jumla ya Shilingi Milioni Moja na laki tatu zimechangwa kupitia Michango yao na mnada wa mazao na vitu mbalimbali vilivyoletwa na akina Mama wa Misikiti tofauti. 

Ujenzi huo, ulioanza miaka ya Nyuma, umekuwa ukisua sua kutokana na Nguvu ya akina mama hawa kuwa kidogo, na Mara nyingi wamekuwa wakifanya matamasha na Harambee mbalimbali ili kuona kama Shughuli ya Ujenzi itasogea, na tayari maandalizi na mipango inaendelea kwa Tamasha kubwa la Mwisho wa Mwaka litakalofanyika Desemba 27 hadi 29 Mwaka huu.
 Pichani Katibu wa UMWAKIKA Hajat Nuriat Kaboyo, akisoma Risala kwa Mgeni Rasmi (hayupo pichani), kubwa ikiwa ni Taarifa ya Ujenzi ilipofikia na kile kinachotarajiwa siku za mbeleni.
 Pichani sehemu ya akina mama waliohudhuria Jaula hiyo, kutoka Misikiti Mitano kama wanavyoonekana wakifuatilia Ratiba.
 Pichani ni Mgeni Rasmi Katika Jaula ya Akina mama wa Kiislam Hajat Faidha Kainamula Mwenyekiti wa UWT Mkoa Kagera, akitoa salaam zake kwa akina mama waliohudhuria Jaula hiyo (hawapo pichani)
 Pichani sehemu ya akina mama waliohudhuria Jaula hiyo, kutoka Misikiti Mitano kama wanavyoonekana wakifuatilia Ratiba.
Pichani Miongoni mwa Mazao na Vitu mbalimbali viliouzwa kwa njia ya mnada ili kukusanya pesa za Ujenzi wa Hospitali ya Mama na Mtoto, inayosimamiwa na Umoja wa maendeleo ya wanawake wa Kiislamu Kagera (UMWAKIKA) Inayojengwa Kata ya Nyanga, Manispaa ya Bukoba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...