Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Amos Nungu akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika wiki ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu. kulia ni Mratibu wa Mkutano wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu, Theophilus Mlaki.

Mratibu wa Mkutano wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu, Theophilus Mlaki akifafanua jambo katika mkutano wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu jijini Dar es Salaam.

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
USHIRIKISHWAJI wenye usawa kwa nchi 15 zilizopo kusini mwa jangwa la Sahara katika Sayansi, Teknolojia na Ubunifu utaleta matokeo chanya katika tafiti za masuala ya kisayansi.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Amos Nungu wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika wiki ya   Sayansi, Tenkolojia na Ubunifu. Katika Mkutano huo amesema kuwa mijadala iliyopo ni katika kushirikiana na kuafikiana ili tafiti zinazofanywa ziwe na matokeo chanya.

Dkt. Nungu amesema kuwa ili kuwe na matokeo chanya ya tafiti za kisayansi lazima kuwe na data wazi ili kuweza kushirikisha nchi nyingine kwaajili ya kupata matokeo mazuri zaidi.

"Katika tafiti na ubunifu kwa maendeleo lazima malengo ambayo serikali na wawekezaji wameyaweka lazima yaonekane hata kwa mwananchi wa kawaida aweze kuona nini kinatokea". Amesema Dkt. Nungu.

Hata hivyo Dkt Nungu amewaomba nchi zilizoendelea kiutafiti kutokuficha baadhi ya vitu katika kufanya utafiti ili nchi za Afrika zikakosa ndio maana mkutano unasisitiza tafiti shirikishi na zenye usawa ili kuwepo na usawa kwa nchi zinazotoa ufadhili na nchi zinazopokea ufadhili katika tafiti za kisayansi.

"Tukiwa na Tafiti wazi na shirikishi mtafiti aweze kuomba takwimu  au data zilezile ambazo mwingine amezitumia akazifanyia kazi  kama sio wazi aliyefanya utafiti kwa mara ya kwanza atazifungia na mwingine atakayetaka kufanya utafiti ule ule lazima aanze mwanzo". Amesema Dkt. Nungu

Katika mjadala huo changamoto iliyojitokeza ni miundombinu ya maabara za kisasa kwa nchi za Afrika ukilinganisha na nchi nyingine.

Ili serikali ipate matokeo mazuri na makubwa lazima wanasayansi kuonyesha kuwa wanaweza na wajitume.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...