Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
WAHITIMU 417 wanatarajiwa kutunukiwa vyeti, astashahada na shahada za kozi mbalimabali zitakazotolewa na Chuo Cha Kodi nchini (ITA) katika mahafali ya 12 yatakayofanyika kesho Novemba 22, Chuoni hapo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkuu wa Chuo hicho Profesa. Isaya Jairo amesema kuwa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philipo Mpango (Mb) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi atakayewatunuku wahitimu hao vyeti na shahada mbalimbali.
Amesema kuwa licha ya kuwatunuku wahitimu hao vyeti na shahada mbalimbali Dkt. Mpango atatoa zawadi kwa wahitimu na wanafunzi waliofanya vizuri zaidi.
Prof. Jairo amesema kuwa wahadhiri waliofanya tafiti mbalimbali katika kipindi cha masomo cha 2018/2019 na tafiti zao kuchapishwa katika majarida mbalimbali ya kitaaluma na katika jarida la Chuo cha Kodi watatunukiwa tuzo katika mahafali hiyo.
Vilevile amesema kuwa katika miaka 12 ya Chuo hicho wanajivunia zaidi katika utoaji wa mafunzo ya forodha na Kodi wakiwa ni Chuo pekee nchini na katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini.
Vilevile amewashauri wahitimu kutumia mafunzo waliyoyapata kuleta tija kwa Jamii na kuwa wazalendo katika kulitumikia taifa hasa kwa wakati huu ambao nchi imejikita katika kujenga uchumi wa kati na viwanda.
Mkuu wa Chuo cha Kodi Profesa. Isaya Jairo akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mahafali ya kumi na mbili ya Chuo hicho yatakayofanyika kesho chuoni hapo ambapo amesema kuwa jumla ya wahitimu 417 watatunukiwa vyeti na shahada mbalimbali kulia ni Mkuu wa mawasiliano wa Chuo hicho Oliver Njunwa, leo jijini Dar es Salaam.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...