Na Woinde Shizza Michuzi Tv, ARUSHA
WAMILIKI
saba wa viwanja katika eneo la Naura jijini Arusha, wamemuomba Rais
John Magufuli, kuingilia kati mgogoro kati yao na Halmashauri ya Jiji la
Arusha uliodumu kwa kipindi cha zaidi ya miaka 32.
Wakizungumza
leo Novemba 21,2019, wamiliki wa viwanja hivyo, wakiongozwa na Issack
Kassam,Manleo Auye,Joshua Kaiza Ndosi, Kanubhai Rameshner Patel na Akber
H.Sanjani, wamesema viwanja hivyo wanamiliki kwa mujibu wa sheria na
wana hatimiliki.
“Tunamuomba
Rais Magufuli atusaidie tupate haki yetu tuliyoitafuta kwa muda mrefu
kwani tumepita katika ofisi mbalimbali za umma tumekuwa tukizungushwa
bila ya kupata msahada wowote,”amesema Sanjani.
“Rais
wetu ni kiongozi anayejali watu hususani wanyonge sisi tunaamini suala
letu atalifanyia kazi hatujawahi kuwa na mashaka na utendaji kazi
wake,”alisema Ndosi.
Kwa
mujibu wa nyaraka za umiliki wa eneo hilo, zinaonyesha kwamba
halmashauri ya Jiji la Arusha iliwagawia maeneo hayo kwa wananchi, kati
ya mwaka 1986/1987 .
Kwa
mujibu wa maelezo ya wamiliki wa viwanja hivyo, walisema baada ya
kupewa maeneo hayo waliomba vibali vya kujenga na kuendeleza maeneo
hayo.
Kwa mujibu wa
nyaraka za siri kutoka kwa wamiliki wa eneo hilo, kwenda Halmashauri ya
Jiji la Arusha inaonesha Julai 25 ,2019, walituma maombi ya kupewa
vibali vya kujenga ukuta katika kiwanja namba 17,kitalu “U”sehemu F.
“Sisi
wamiliki halali wa kiwanja tajwa hapo juu chenye namba 10258, ni muda
mrefu sasa hatujaendeleza viwanja hivi kulingalina na mgogoro uliopo
katika eneo hilo, hata hivyo tumekuwa tukilipa kodi ya serikali hadi
leo,”
“Kwa barua hii
tunaleta ombi kwako la kuomba kibali cha ujenzi wa ukuta kuzunguka eneo
letu ili tuweze kuendelea na mipango iliyopo katika kiwanja bila ya
kusumbuliwa,”imesema sehemu ya barua.
Aidha
walisema baada ya mgogoro huo kudumu kwa muda mrefu mwaka 1996,
walipokea barua ya kurejeshewa viwanja hivyo. Mwaka 1999, Wizara ya
Ardhi kipindi hicho,ilitoa agizo kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa
Arusha,Mkurugenzi wa halmashauri na Meya wa Jiji la Arusha kurudisha
maeneo hayo kwa mahusika ili wayaendeleze.
“Viwanja
hivi tuna hatimiliki kwa vipindi vyote tumeomba vibali vya
kuviendeleza nakujenga lakini hatukupewa kilichotokea ofisi zote za
serikali tulizopita kudai haki yetu wametuzungusha bila ya kutupa
masahada wowote,”aliongeza
Kwa
mujibu wa hatimiliki hiyo, inaonyesha kuwa wamiliki wa maeneo hayo,
wameshailipa halmashauri ya Jiji la Arusha kodi hadi kufikia mwaka 2020.
“Chakushangaza
maeneo yetu yamekodishwa kwa kampuni moja ya ujenzi kutoka nchini China
bila ya sisi kujulishwa wakati tunamiliki kisheria,”alisema.
“Taarifa
tulizonazo ni kwamba kampuni hii ya ujenzi inalipa kodi kiasi cha
sh.milioni 50, kwa mwezi tunataka kufahamu ni nani aliyekodisha eneo
letu pia anayopokea kodi wakati wahusika tupo ,”alisema
Kwa
mujibu wa nyaraka hizo, zinaonyesha Issack Kassam anamiliki ploti namba
19, bloku “U”,eneo F, Manleo Auye ploti namba 16, bloku “U”eneo F,
Joshua Kaiza Ndosi ploti namba 21, bloku “U”eneo F, Kanubhai Rameshner
Patel ploti namba 22, bloku “U” eneo F.
Muonekano wa eneo la viwanja lenye mgogoro kati ya wamiliki ma
Halmashauri ya Jiji la Arusha, na viwanja hivyo vimekodishwa kwa kampuni
ya ujenzi kutoka China
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...