Na.Khadija seif, Michuzi TV

WAMILIKI wa kumbi za mikutano na starehe wametakiwa kuutangaza utalii wa ndani pindi wageni na wenyeji wanapotembelea sehemu hizo.

Akizungumza na Michuzi tv Meneja wa Hoteli ya Serena iliyopo jijini Dar es salaam Shaban Karuse amesema wakati mwengine tusione wasanii tu na watu maarufu ndio wenye dhamana ya kuutangaza utalii na vivutio vingine peke yao bali hata wamiliki wa kumbi wanatakiwa waione fursa hiyo mara moja.

"Kwa kuthamini mchango wa utalii sisi tumeamua kunyanyua sanaa ya ubunifu ikiwemo ya mavazi na vitu mbalimbali na ukifika hoteli yetu ya serene iliyopo hapa Dar es salaam utapata vitu vya kibunifu na vya asili ya kitanzania na hata nakshi nakshi na mapambo yaliyopambwa katika hoteli hii ni ya asili ya kitanzania mfano milango,viti pamoja vitu vingine ni vya kinyumbani.

Aidha, Karuse amefafanua mbali na vitu hivyo karuse ameeleza kuwa hoteli hiyo imeona fursa pekee ya kunyanyua na kukuza Sanaa ya ubunifu na ndio maana kila siku ya jumamosi kunakuwepo wabunifu na meza zao ili kuuza bidhaa zao kwa watu wanaofika hotelini.

"Ipo wazi kuwa kila jumamosi ni sikukuu ya wabunifu kwa hapa hoteli ya Serena na hakuna malipo yoyote kwa mbunifu anaetaka kushiriki katika gulio hilo,"

Pia ametoa wito kwa watanzania kuwa wazalendo na kuthamini vitu vya kinyumbani na kuacha kununua nguo kutoka nchi za wenzetu kwani kununua vya kinyumbani ni mojawapo ya kuwa mzalendo.

"Batiki,vitenge,kaniki ,vibwaya ni mavazi ambayo yanapatikana hapa nchini na watalii wakifika hapa nchini wanaonyesha uzalendo kwa kuvinunua kwanini sisi wenye tusivinunue na tusiwatie moyo wabunifu wetu ambao wapo na wanatengeneza vitu vizuri na vya kiasili na vyenye ubora,"

Hata hivyo karuse amesema kwa kuthamini mchango wa wabunifu hoteli hiyo imeamua kudhamini wiki ya Maonyesho ya  12 ubunifu wa Mavazi (Swahili fashion week) ya mbunifu mkongwe hapa nchini Mustafa Hassanali.
Meneja wa hoteli ya serena ya jijini Dar es salaam akitolea ufafanuzi juu ya kutangaza utalii kwa wamiliki wa kumbi za mikutano na starehe pamoja na kudhamini wiki ya Maonyesho ya 12 ya ubunifu wa mavazi ya Mustafa Hassanali yanayotarajia kuanza desemba 6 hadi 8 mwaka huu jijini Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...