Na Said.Mwishehe, Michuzi TV-Mwanza

UONGOZI wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania  (TPA), Kanda ya Ziwa jijini Mwanza umesema umeweka mikakati ya kukomesha utitiri wa bandari bubu karibu 300 katika ziwa Victoria.

Umesema katika kuhakikisha bandari ya Kanda ya Ziwa anaongea ,ukusanyaji wa mapato kutokana na huduma inazotoa,umeamua kuwa na malengo ya kuhakikisha bandari hizo zinatambulika na kuwa vyanzo cha mapato.

Akizingumza leo akiwa ofisini kwake jijini Mwanza, Meneja wa Bandari za Ziwa Victoria, Morris Machindiuza amesema wameamua kukabiliana na changamoto ya uwepo wa bandari bubu na watazichukulia hatua kwa mujibu wa sheria ambayo inaeleza wazi shughuli zote upakiaji,upakuaji na usimamizi wa shughuli za bandari ziko chini ya mamlaka ya TPA.

Hata hivyo amesema kuwa pamoja na kukabiliana na bandari bubu, pia TPA imepewa jukumu ya kuendeleza bandari na kuendesha, kutangaza huduma za bandari kwa kushirikiana na sekra binafsi katika uendeshaji wa bandari.

“Katika mwambao wa Ziwa Victoria TPA inamiliki na kusimamia bandari kubwa za Mwanza Kaskazini na Kusini, Nansio, Kemondo Bay, Bukoba na Musoma pia kuna bandari zingine ndogo za mwambao zaidi ya 15 ambazo zote tunazihudumia kwa kuwa chini ya usimamizi wetu,” amesema Machindiuza.

Pia amesema TPA inaendesha Bandari Kavu ya Isaka ambayo inamilikiwa na Shirika la Reli Tanzania ambapo kuwa ghala kubwa lenye uwezo wa kuhifadhi shehena ya tani 3,000, yadi ya makasha na yadi ya Rwanda yenye eneo la ekari 17.05.

Kuhusu hali ya mapato amesema imepanda kutoka Sh milioni 600 hadi kufikia Sh bilioni 1.4 jambo ambalo ni la kutia moyo katika uendeshaji wa shughuli za bandari.
 
“Kwa sasa Serikali ya Awamu ya Tano mkakati mkubwa ni kukusanya mapato ya ndani, nasi TPA kama wadaui taasisi muhimu tunalizingatia hilo kwa kuhakikisha tunatafuta wafanyabishara ambao ilin waweze kutumia bandari zetu,” ameongeza Machindiuza
 Moja ya meli ya mizigo ambayo imekuwa ikitumika kubeba mabehewa yenye konteza za mizigo ambayo inatoka jijini Dar es Salaam kwa kutumia reli ya kati na kisha kuingizwa kwenye meli hiyo kuelekea nchini Uganda.
 Meneja wa Bandari za Ziwa Victoria Morris Machimbiuza akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Desemba 5, mwaka 2019 kuhusu mikakati iliyowekwa katika kuhakikisha wanaendelea kuboresha utoaji huduma katika bandari za kanda ya Ziwa.Pia amezungumzia mafanikio ambayo yamepatikana katika miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano.
 Meneja wa Bandari za Ziwa Victoria Morris Machimbiuza akiwa na baadhi ya maofisa wa Bandari za Ziwa Victoria pamoja na waandishi wa habari baada ya kuonesha daraja la reli ambalo linatumika kupitisha kontena kutoka katika behewa za treni kwenda katika meli za mizigo bandarini hapo.

 Sehemu ya reli inayotumika kwa ajili ya kupitisha behewa za mizigo kuingizwa kwenye meli za mizigo katika Bandari ya Kanda ya Ziwa jijini Mwanza.
 Daraja la reli ya kupitisha mabehewa yenye mizigo kupandishwa katika meli kwa ajili ya kusafirisha katika nchi jirani ambazo zinatumia bandari ya Ziwa Victoria kusafirisha mizigo yake.
 Muonekana wa sehemu ya Bandari ya Kanda ya Ziwa huku baadhi ya watumishi wa bandari hiyo wakionekana kwa mbali wakiendelea na majukumu yao ya kila siku.PICHA ZOTE NA SAID MWISHEHE

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...