Katika kutambua afya ni suala muhimu sana kwa maendeleo ya jamii, Benki ya NMB imekabidhi vitanda 15 vyenye jumla ya thamani ya milioni 45 kwa ajili ya chumba cha watoto wagonjwa waliopo kwenye uangalizi maalum (ICU) katika hospitali za Muhimbili na Mloganzila za jijini Dar es Salaam.

Akikabidhi msaada huo kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, Afisa Mkuu wa Mahesabu wa Benki ya NMB, Juma Kimori, alibainisha kwamba thamani ya vitanda vyote ni Sh. Milioni 45 huku  akifafanua kuwa kitanda kimoja cha ICU ya watoto kimegharimu Sh. Milioni 7.5 na kuahidi kuendelea kushirikiana na serikali kuboresha sekta ya afya.

Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Zuhura Mawona, aliishukuru na kuipongeza NMB kwa msaada huo na kuiomba iendelee kutoa msaada zaidi kwa ajili ya chumba hicho maalum kwa watoto.

“Tulipeleka maombi NMB na wametujibu hatuchoki, tunaendelea kuwaomba mtushike tena mkono, maana mahitaji ya vitanda katika chumba hicho muhimu cha kuokoa maisha ya watoto ni mkubwa, bado tunahitaji vingine saba mkiguswa tena mtukumbuke.

“Kabla ya wodi hii kuanza watoto walikuwa wanachanganywa kwenye ICU za wakubwa na kule vitanda sio sawa na hivi tulivyopokea vya NMB hata sisi  wahudumu hatupati tabu sana kuvinyanyua wala mgonjwa haumii kila kitu kinasetiwa kwenye umeme asanteni sana NMB,” alisema Mawona aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Hospitali ya Taifa Muhimbili.#NMBKaribuYako
Afisa Mkuu wa Ukaguzi wa Mahesabu ya Ndani wa Benki ya NMB, Juma Kimori akimkabidhi Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto; Mh. Ummy Mwalimu masada wa vitanda 15 kwa ajili ya chumba cha watoto wagonjwa waliopo kwenye uangalizi maalum(ICU) katika hospitali za Muhimbili na Mloganzila za jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto; Mh. Ummy Mwalimu na Afisa Mkuu wa Ukaguzi wa Mahesabu ya Ndani wa Benki ya NMB, Juma Kimori  wakiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wao kutoka hospitali za Muhimbili na Mloganzila.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...