Mkurugenzi wa Taasisi ya TSDT Sosthenes Kewe akizungumza wakati wa kufunga tamasha la Data Tamasha kwa mwaka 2019 ambapo amewashauri vijana kutumia maarufa ya kidigiti vyema katika kujenga taifa, leo jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Tanzania Data Lab, Dkt. Blandina Kilama akitoa cheti cha pongezi kwa mmoja wa washiriki waliohudhuria Tamasha hilo, ambapo amesema kuwa makundi maalumu wakiwemo vijana, wanawake na watu wenye ulemavu ni muhimu kushirikishwa katika ukusanyaji wa taarifa na takwimu, leo jijini Dar es Salaam.

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

IMEELEZWA kuwa ushirikishwaji wa makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ni katika kukusanya na kutumia takwimu na taarifa kwa jamii ya sasa ni muhimu na yenye kuleta tija kwa jamii na hiyo ni kutokana na sekta ya kidigitali kukua na kuhitaji kuzibwa kwa ombwe la ushirikishwaji lililopo ili kujenga taifa imara.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kufunga tamasha la Data Tamasha ambalo limewakutanisha watu wa kada mbalimbali Mkurugenzi wa  Financial Sector Deepening Trust (FSDT) Sosthenes Kewe  amesema kuwa tamasha hilo limekuwa moja ya  tamasha kubwa na kueleza kuwa washiriki  lazima wametoka na  maarifa ambayo  yatawasaidia katika kutatua changamoto mbalimbali katika jamii zao.

Kewe amesema kuwa baada ya kupata maarifa hayo ni vyema washiriki  watumie changamoto wanazokutana nazo kama kama fursa na  wakaibadilishe jamii na taifa kupitia maarifa hayo na hiyo ni pamoja na kufanya gunduzi zenye tija katika jamii.

Aidha amesema kuwa sekta ya uchumi inaenda sambamba na gunduzi hivyo wanafunzi lazima wajikite katika kufanya hilo kwa kuwa nafasi hiyo kwao ipo wazi na kwa kufanya hivyo  wataacha alama kwa kizazi  cha sasa na baadaye na historia yao haitofutika.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya taasisi ya Tanzania Data Lab  Dkt. Blandina Kilama amesema siku tatu za Tamasha hilo zimetumika katika kujifunza mambo mengi ikiwemo ushiriki wa wanawake, watu wenye ulemavu na vijana hivyo kilichobaki ni kutumia vyema maarifa hayo ambayo wanaamini yataleta Mabadiliko chanya.

Amesema kuwa katika kusheherekea siku ya takwimu na taarifa wataalamu kutoka ndani na nje ya nchi wametoa uzoefu ikiwa ni pamoja na matumizi ya vyombo mbalimbali ikiwemo ofisi ya takwimu na taarifa katika kushirikiana na kupeana taarifa za kitakwimu.

Vilevile amesema kuwa siku hizo tatu zimekuwa na faida kwa vijana ambapo wamepata uzoefu na njia mbalimbali za ubunifu ambazo zitawasaidia kijijenga na kuleta matokeo chanya katika jamii na taifa kwa ujumla.

Pia Mkurugenzi wa Tanzania Data Lab, Stephen Chacha amesema kuwa wamekuwa wakisherekea siku ya takwimu na taarifa kila baada ya miaka miwili ila kuanzia mwakani wataadhimisha siku hiyo kila mwaka na hiyo ni kutokana na mwamko na mahitaji ya wadau katika kujenga tasnia hiyo yenye tija kwa jamii.

Chacha ameishukuru Serikali kupitia ofisi ya Takwimu kwa  kwa ushirikiano wanakutoa katika kuendeleza mbele tasnia hiyo muhimu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...